HIZI HAPA SENTENSI 8 ZA MHESHIMIWA LOWASSA AKITANGAZA NIA YA URAIS TANZANIA, SAUTI YAKE IKO HAPA AKIHUTUBIA HUKO ARUSHA



May 30 2015 inakuwa siku ambayo inaingia kwenye Historia kubwa kwenye ishu za siasa Tanzania.. Bado miezi michache ufanyike Uchaguzi Mkuu, mmoja ya watu ambao walitajwa sana na kuwa kwenye headlines kubwa kwenye vyombo  vya habari ni Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa.

Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid katikati ya Jiji la Arusha umeshuhudia kwa mara nyingine kujaa kwa watu ambao walikuja kwa ajili ya kushuhudia Mbunge huyo akitangaza nia rasmi kabisa kwamba atagombea Urais mwaka huu.
Watanzania wanahitaji mabadiliko, nina uwezo wa kusimamia mabadiliko hayo.. Mwalimu Nyerere alisema Watanzania wasipoyapata mabadiliko hayo ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM. Sina shaka tukijipanga vizuri ndani ya CCM tunaweza kuwapa Watanzania mabadiliko wanayoyataka”>>> Edward Lowassa.
Nchi yetu inahitaji viongozi wenye sifa hizi.. uongozi wenye uthubutu usioogopa kufanya maamuzi magumu, uongozi usioyumba.. Aweze kuwaunganisha Watanzania na kutoa utofauti kati ya walio nacho na wasio nacho“>>> Edward Lowassa.
Nina hamu, nina shauku na nina uwezo wa kuiongoza Tanzania… Ninaamini nina kila kigezo cha kuibeba dhamana ya nchi yetu.. Katika vitu ninavyojivunia ni pale nilipoenda kupigana vita ya Kagera, nilishiriki kikamilifu nikiwa miongoni mwa askari wa mbele kuikomboa nchi yetu, muwaulize wengine waliwahi hata kufika Kagera?
Kwa wingi wa rasilimali tulizonazo tuna kila sababu ya kuwa ombaomba… Haya ninayoyaeleza ndio msingi wa utendaji wa Serikali nitakayoiongoza nikichaguliwa.. nimeamua kugombea Urais ili kupambana na umaskini.. Uongozi wangu utaleta mchakamchaka wa maendeleo”– Edward Lowassa.
Najua Watanzania wangapi wanaishi kwa bodaboda, mama ntilie.. hawa ni rafiki zangu hawatafukuzwa barabarani.. ni raia wa Tanzania wanaostahili kula kama wewe
Kwenye michezo tumechoka kuwa kichwa cha mwendawazimu, tutaibadili hali hii kwa kasi sana“>>> Edward Lowassa.
Sauti yake iko hapa, ukiplay utasikia hotuba yake yote

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post