HIZI HAPA TAKWIMU MUHIMU ZA WAZEE NCHINI TANZANIA


Zifuatazo ni takwimu muhimu za wazee nchini Tanzania.Takwimu hizi zimetolewa juzi na mratibu wa Chama Cha Wataalam Viongozi Wanawake wa Kilimo na Mazingira (TAWLAE) Eliasenya Nnko(PICHANI) wakati wa kikao cha Waandishi wa Habari klichofanyika mjini Shinyanga kuhusu kuongeza na uhamasishaji juu ya sera ya mikakati ya kuboresha maisha ya wazee nchini.
****

TAKWIMU MUHIMU ZA WAZEE
1.Mzee kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Wazee ni wenye umri wa Miaka 60+ 

2.Kwa Mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi - 2012, Wazee Miaka 60 na kuendelea ni asilimia 5.6 (2,507,568 Kati yao 1,307,358 ni Wanawake na 1,200,210 Wanaume.
 
3.Mikoa ya Kilimanjaro, Pwani, Lindi na Mtwara, inaonyesha idadi kubwa ya wazee ikiwa na asilimia 7,  6.7,  6.3 na 6.2 kama inavyo fuatana.
 
4.80% ya wazee wanaishi Vijijini.

5.50% ya yatima wote Tanzania wanatunzwa na wazee, Mara nyingi ni wazee Wanawake. 

6.Wazee 2,866 waliuawa kwa imani za ushirikina katika Mikoa 10 kwa kipindi cha Miaka 5, - wastani wa mauaji 573 kila Mwaka.

7. Karibu asilimia 60% ya Vifo vyote miongoni mwa wazee wa umri wa Miaka  60 na kuendelea katika baadhi ya Wilaya Nchini vinasababishwa na Magonjwa yasiyo ya kuambukizwa (NCDs).

CHANGAMOTO  ZINAZOWAKABILI WAZEE WA TANZANIA
  1. Changamoto zinazohusiana na huduma za afya.
a)Watumishi wa Afya kutoelewa vizuri mahitaji ya Kiafya ya wazee – (Geriatric Care).

b)Upungufu wa Madawa na huduma nyinginezo katika Vituo vya Afya/Hospitali za Serikali.

c)Tatizo la upatikananji wa Dawa/Matibabu ya Magonjwa yanayowasibu wazee (NCDs), Kisukari, Moyo, Miguu, Macho n.k.

d)Lugha zisizo rafiki kwa wazee.

e)Wazee wanakataliwa huduma bila malipo.  

f)Ukosefu wa pato kulipia gharama za usafiri kwenda Hospitali/kununua Dawa.

g)Matibabu bila malipo kuwa kwenye Hospitali za Serikali tu (Zaidi ya 40% ya Tiba nchini zinatolewa na watu binafsi).

h)Maagizo ya Serikali kwa kila Halmashauri kuwa na Kitengo na Mratibu wa Afya wa wazee kutotekelezwa.

  1. Changamoto kuhusiana na Ukiukwaji wa Haki za wazee.
a)Mauaji na manyanyaso yatokanayo  na tuhuma za kishirikina. 

-Mwaka 2011- 517
-Mwaka 2012 - 642
-2013- Mpaka June - 302

b)Kupoteza mali zao na haki za kurithi. 

c)Kupigwa, kupuuzwa na kutolewa maneno ya kashifa.

d)Kufukuzwa kwenye maeneo yao. 

e)Lugha na matendo ya kibaguzi kwa wazee. 

  1. Changamoto za Kipato
a)96% hawako kwenye mfuko wowote wa hifadhi jamii. (wakulima, wavuvi Wafugaji n.k hawapati Pension akizeeka anaangaika sana).

b)Ubaguzi katika taasisi za fedha – vigumu kupata mkopo/ mtaji.
 
c)Wazee ambao ni 5.6% wanatunza zaidi ya nusu ya yatima wote (2 milion).

d)Kaya zenye wazee na watoto umaskini wao huko juu kwa 22.4% ya umaskini Kitaifa (HBS 2007).
 
Kikwazo ni nini katika kutatua Changamoto za Wazee Nchini
a)Mtizamo hasi wa Jamii Kwa wazee. 

b)Sera na matamko kuhusu wazee kutotungiwa Sheria. 

c)Upungufu wa takwimu zinazohusu wazee. 

d)Kukosa uwakilishi katika vyombo vya maamuzi (WDC, Full Council, Bunge).

e)Baadhi ya wenye mamlaka kutopenda kuwapatia wazee hata yale yaliyo kwenye Sera na miongozo ya taifa mfano-Mikopo Kina mama.  

f)Kutoanzishwa/kuimarishwa kwa mabaraza huru ya wazee kuwapa sauti.
 *******************************************

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post