Kamanda wa polisi Mkoa Polisi Mkoa wa Simiyu Gemuni Mushy akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) |
Jeshi la
polisi Mkoani Simiyu linamshikilia Chigila Gilala mkazi wa kijiji cha Bukigi
kata ya Malampaka wilayani Maswa (45) kwa kosa la kukutwa na viungo
zinavyodhaniwa kuwa vya binadamu likiwemo fuvu la kichwa.
Mtuhumiwa huyo
ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM katika kijiji hicho na Mganga wa tiba asili alikamatwa
nyumbani kwake, baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa alikuwa amewahifadhi majambazi kwa ajili
kugangwa (kuzindikwa).
Akitoa taarifa kwa waandishi wa kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Simiyu Gemini Mushy
alieleza kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa mwenyekiti huyo lilitokea Mei 9 mwaka
huu majira ya saa 11 jioni katika kijiji
hicho.
Kamanda
Mushy alisema kuwa askari wakiongozwa na mkuu wa upelelezi katika wilaya ya Maswa walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwepo kwa majambazi nyumbani kwa
mganga huyo, kuwa alikuwa amewahifadhi kwa ajili ya kuwazindika.
Alisema baada ya kupata taarifa hizo walifanya msako nyumbani kwa mwenyekiti huyo,
ambapo alibainisha kuwa walianza kufanya
upekuzi ndani na nje ya nyumba.
“Wakati
wakifanya upekuzi huo walikutana na mfuko wa sandarusi ukiwa chini ya lundo la
kuni nje ya nyumba ya mwenyekiti
huyo..na katika mfuko huo kulipatikana fuvu la kichwa pamoja na mifupa ya
mikono au miguu vinavyodhaniwa kuwa ni viungo vya binadamu” Alisema Mushy.
Kamanda alieleza
kuwa jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi kama kweli viungo hivyo ni vya binadamu
na kama anahusika na uwepo wa viungo hivyo kutokana na kukutwa nje ya nyumba yake.
Wakati huo
huo kamanda Mushy alibainisha kuwa jeshi hilo linamshikilia Gandula Mashimo mkazi wa kijiji cha
Longalombogo kata ya Migato wilaya ya Itilima Mkoani hapa kwa kukutwa na
Bunduki ya kivita SMG na risasi 273.
Alisema kuwa
mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi majira ya saa 3:30 usiku kijijini hapo, akiwa
embeba siraha hiyo pamoja na risasi katika mfuko wa sandarusi.
Alisema mtuhumiwa alikamatwa baada ya wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi wilayani
humo, ambapo alikamatwa akiwa njiani kuelekea kusikojulikana.
Mushy
alieleza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini washirika wake, ikiwemo na
matumizi ya silaha hiyo, huku akitoa wito kwa wananchi mkoani hapa kutoa
taarifa za watu wanaowahisi kuwa siyo wema katika maeneo yao.
Aidha alitoa
onyo kwa ambaye anamiliki silaha bila kibali rasmi, kuwa ajisalimishe pamoja na
silaha yake mara moja kabla ya msako mkali kuanza.
Social Plugin