Ripoti
kutoka Bujumbura zinasema kuwa kamanda mmoja wa kijeshi ametangaza kuwa
hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa Burundi.
Mkuu huyo wa zamani wa shirika la kijasusi la Burundi ametangaza kuwa Rais Pierre Nkurunziza amepinduliwa baada ya machafuko ya zaidi ya wiki mbili yaliyozuka baada ya Nkurunziza kuamua kugombea urais kwa muhula wa tatu mfululizo.
Meja Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza leo kupitia redio ya taifa jijini Bujumbura kwamba, kuanzia sasa Rais Pierre Nkurunziza si rais tena wa Burundi.
Amesema, serikali imevunjwa, makatibu wa kudumu wa mawaziri wataendesha masuala ya nchi hiyo hadi tangazo jingine litakapotolewa.
Tangazo la Meja Jenerali Niyombare limekuja baada ya jeshi la Burundi kuzizingira ofisi za redio ya taifa katika jiji la Bujumbura. Mapema leo polisi wa Burundi wamefyatua risasi na mabomu ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji waliojaribu kulivamia bunge.
FUATILIA HAPA JINSI MATUKIO YANAVYOENDELEA MPAKA SASA HIVI
20:41 Ndege haziruhusiwi kutua ndani ya uwanja huo
20:40 Mwandishi wa BBC aliyeko Bujumbura anasema kuwa taa katika uwanja wa ndege zimezimwa.
20:31Meja jenerali Godefroid Niyombarekuwa ametangaza kufungwa uwanja wa ndege wa Bujumbura.
20:30 Meja jenerali Godefroid Niyombarekuwa ametangaza kufungua kwa mipaka yote ya Burundi.
20:29 Kundi hilo limekanusha tangazo la Meja jenerali Godefroid Niyombare kuwa ameipindua serikali ya Nkurunzinza
20:28 Kundi la wanajeshi wanomuunga mkono Nkurunzinza wangali wanadhibiti Ikulu na kituo cha redio ya taifa''AFP''.

Saa>>20:42 Hakuna uhakika iwapo ndege ya rais Nkurunzinza itaruhusiwa kutua
20:41 Ndege haziruhusiwi kutua ndani ya uwanja huo
20:40 Mwandishi wa BBC aliyeko Bujumbura anasema kuwa taa katika uwanja wa ndege zimezimwa.
20:31Meja jenerali Godefroid Niyombarekuwa ametangaza kufungwa uwanja wa ndege wa Bujumbura.
20:30 Meja jenerali Godefroid Niyombarekuwa ametangaza kufungua kwa mipaka yote ya Burundi.
20:29 Kundi hilo limekanusha tangazo la Meja jenerali Godefroid Niyombare kuwa ameipindua serikali ya Nkurunzinza
20:28 Kundi la wanajeshi wanomuunga mkono Nkurunzinza wangali wanadhibiti Ikulu na kituo cha redio ya taifa''AFP''.
19:00 Katibu mkuu wa umoja wa
Mataifa Ban ki-Moon amewataka wahusika wakuu nchini Burundi kuweka
uhasama baina yao kando ili kulinda taifa.
Polisi waliokuwa wakipigana na waandamanaji wameondoka
18:53 Kiongozi wa ''Mapinduzi'' kwa upande wake Meja Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza kufungwa kwa mipaka.
18:45 Mwandishi wa BBC huko Bujumbura Kazungu Lozy anasema watu wangali wanasheherekea.
18:40 Rais Nkurunzinza ameingia ndani ya gari lake na kuondoka mjini Dar es Salaam akionesha dalili kuwa yuaelekea Burundi
18:37
Kiongozi wa ''Mapinduzi'' kwa upande wake Meja Jenerali Godefroid
Niyombare ameamrisha wanajeshi kuzuia rais Nkurunzinza kutua Burundi
18:30 Rais Pierre Nkurunziza anatarajiwa kuhutubia taifa baada ya kurejea kutoka Tanzania amesema msemaji wake Willy Nyamitwe.
18:25 Generali Niyombareh ametoa amri kwa majeshi kuungana na kulinda viwanja vya ndege kote nchini humo
18:20 Generali aliyeongoza
''Mapinduzi'' leo asubuhi amewataka maafisa wa jeshi na polisi kufanya
kazi kwa pamoja ilikulinda usalama wa nchi hiyo.
18:15 Viongozi wa kanda ya Afrika wametaka makundi hasimu kutulia na kukubali hali ya kikatiba Kurejea
18:06 Rais wa Tanzania amekashifu ''mapinduzi'' yaliyotoke leo huko Burundi
18:05 Rais amesema hayo katika mkutano wa upatanishi wa viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki
18:01 Ujumbe wa mtandao wa facebook wa urais nchini Burundi umekanusha kutokea kwa ''Mapinduzi''.
18:01 Viongozi hao wanakutana dar es salaam kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi
18:01 Rais Jakaya Kikwete amesema hayo katika mkutano wa upatanishi wa viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki
18:00 Rais wa Tanzania amekashifu ''mapinduzi'' yaliyotoke leo huko Burundi
17:55 Msemaji wa rais Nkurunzinza ameiambia BBC kuwa asilimia 95 ya taifa hilo ingali salama na wala hakuna tashwishi.
17:50 Manuari zaidi zaonekana barabarani mjini Bujumbura
17:45 Ujumbe wa mtandao wa facebook wa urais nchini Burundi umekanusha kutokea kwa ''Mapinduzi''.
17:30 Msemaji wa rais
Nkurunziza,Willy Nyamitwe ameiambia BBC kuwa rais huyo angali
madarakani na kuwa hajaondolewa madarakani
17:22 Redio ya taifa ya Burundi inasema kuwa rais Nkurunzinza angali Madarakani na kuwa hakujakuwa na ''mapinduzi''
Raia wakikumbatiana katika bustani la uhuru Bujumbura
17:20 Maafisa wa jeshi wanaolinda kituo cha taifa cha redio wamewaonya watangazaji wasitangaze kuwa kuna ''mapinduzi''
17:05
Mwandishi wa BBC aliyeko huko Ruth Nesoba anasema kuwa waandamanaji
wamefululiza hadi kwenye vituo vya polisi na magereza yaliyokuwa na
mahabusu waliokamata kwa kuandamana na kuwaachilia huru
17:00 Redio ya taifa inasema kuwa bado rais Nkurunzinza angali madarakani.
16:50 Kituo hicho cha redio cha ''African Public Radio'' kinapeperusha tangazo la kupinduliwa kwa serikali ya rais Nkurunzinza
16:40 Redio iliyokuwa imefungwa na serikali ya rais Nkurunzinza kwa kupeperusha habari za maandamano imefunguliwa upya.
16:30 Mwandishi wa BBC Cyriac Muhawenay aliyeko Bujumbura anasema raia wanaonekana kuwa na furaha.
16:20 Picha za raia wakiwa wamekwea vifaru vya kijeshi
16:08 Watu wanaonekana wakininginia kwenye vifaru vya jeshi.
16:05 Afisi ya urais nchini Burundi imetangaza kwenye mtandao wake wa twitter kuwa ''hali ni Shwari''
16:00 Majeshi wameonekana nje ya kambi za kijeshi mjini Bujumbura.
15:58 Viongozi wa jeshi wamewaamrisha maafisa wa polisi kuondoka mabarabarani.
15:55 Mwandishi Sonia Rolley, wa Radio France International anasema
kuwa halaiki ya raia wamefika nje ya kituo hicho wakishangilia matukio
hayo
15:50 Waandamanaji wanasemekana kuambatana na wanajeshi kuelekea katikati ya mji mkuu wa Bujumbura.
15:45
Rais Pierre Nkurunziza ambaye analaumiwa kugombea urais kwa muhula wa
tatu, anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo, kusikiliza hoja za viongozi
wenzake.
15:40 Mwandishi wa BBC aliyeko Bujumbura Maud Julien anasema kuwa Miili ya watu watatu imeonekane katika barabara za Bujumbura.
15:36 Viongozi wote wa kanda ya Afrika Mashariki na kati wako Dar es Salaam kwa mwaliko wa rais Kikwete.
15:35 Rais Nkurunzinza yuko mjini Dar es Salaam Tanzania kuhudhuria
mkutano wa kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisasa uliokuwa ukiendelea
Burundi.
15:30 Maelfu ya raia wa Burundi waandamana a
mabarabarani mjini Bujumbura wakishangilia tangazo hilo la
''kutomtambua'' rais Nkurunzinza.
15:20 Jenerali huyo
aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza
alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.
15:10
Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa
Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.
15:05 Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.
15:00 taarifa zaibuka kutoka Burundi kuwa rais Nkurunzinza ameng'olewa'' madarakani.
Ripoti kutoka Bujumbura zinasema kuwa kamanda mmoja wa kijeshi
ametangaza kuwa hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa Burundi
Meja Jenerali Godefroid
Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa
kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi itakayotawala taifa hilo kwa
kipindi cha mpito.
Kulingana na taarifa iliyopeperushwa na redio Isanganiro, serikali ya Nkurunziza imeon'golewa madarakani.
Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu
wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa
Nkurunziza.
Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi
februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani
mbali na sheria za kimataifa.
Kwa sasa rais Nkurunziza yuko
nchini Tanzania alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda hii
ya Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu
Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.
Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.
Tayari wanajeshi wameshika doria nje ya makao makuu ya runinga ya taifa.
Rais Nkurunzinza alikuwa amepuzilia mbali maombi ya kuahirisha uchaguzi huo.
Duru kutoka Burundi zinasema kuwa raia wameshajitokeza mabarabarani wakishangilia kauli hiyo ya ''Mapinduzi''
CHANZO-BBC
Social Plugin