Hii ishu ilikuwa kama utani hivi, zikaanza stori kwamba D’Banj
anadaiwa na jamaa mmoja Nigeria.. baadae tukasikia kwamba jamaa
anayemdai ametishia kumshtaki.. leo hii story ina mwendelezo wake.
Henry Ojogho ambaye ni makamu Mwenyekiti wa Broron Group and MindHub Technologies amesema anaidai Kampuni ya DKM Media ambayo inamilikiwa na D’Banj
kiasi cha kama Naira Mil.60 ambazo ukiziweka kwenye hela yetu ni kama
Tshs. Mil. 600 hivi.. kesi ilifika Mahakamani na kuanza kusikilizwa
Lagos Nigeria, March 30 2015.
Siku hiyo ya kwanza kesi kusikilizwa Mahakamani wote wawili, yani D’Banj mwenyewe pamoja na Henry hawakuwepo Mahakamani.
Kesi ilisogezwa mbele na itasikilizwa tena Mahakamani siku mbili zijazo, yani May 7 2015.. D’Banj ni moja ya mastaa makubwa wenye mafanikio Africa ambaye anafanya kazi za kimuziki Marekani chini ya lebo ya G.O.O.D Music ambayo inamilikiwa na rapper Kanye West.
Kwenye list ya mastaa wa muziki wenye utajiri mkubwa zaidi Africa D’Banj yuko #3.. Hili deni ni kweli kashindwa kulipa au ni nini kinaendelea hapo??
Social Plugin