Hatimaye
mgomo wa madereva umemalizika baada ya kufikia makubaliano kati yao na
serikali juu ya namna ambavyo madai yao yatakavyoshughulikiwa na
serikali.
Awali kabla ya kufikia makubaliano hayo askari walianza kutoa
baadhi ya mabasi chini ya ulinzi mkali wa polisi wa kikosi cha kutuliza
ghasia FFU pamoja na askari wa usalama barabarani zoezi ambalo baada ya
muda lilionekana kukwama kwa kile baadhi ya madereva waliokuwa kituoni
hapo kudai kuwa mgogoro huo hauwezi kumalizika kwa kutumia nguvu.
Harakati za kumaliza mgomo huo zilianza mapema alfajiri kwa vikao
vilivyofanyika kituoni hapo kati ya madereva na wamiliki wa mabasi na
baadae mchana alifika mkuu wa wilaya ya kinondoni ambaye kabla ya
kufikia muafaka huo wakiwa katika mazungumzo vurugu zilizuka gafla
ambapo baadhi ya vijana walianza kurusha mawe kuelekeza kwa viongozi hao
wakiwemo wakuu wa polisi na waandishi wa habari na baadhi ya watu
kujeruhiwa hali iliyowalazimu polisi kutumia mabomu ya machozi.
Mara baada ya kufikia makubaliano hayo katibu wa chama cha madereva
akazungumza na umati wa madereva na abiria waliokuwa kituoni hapo na
kutaja madai waliotiliana saini na serikali huku mkuu wa wilaya ya
kinondoni akielezea namna serikali itakavyoshughulikia suala hilo na
yeye atafanya nini endapo halitafanikiwa.
Hata hivyo baada ya mabasi hayo kuanza kutoka ndani ya kituo hicho
baadhi yake yalionekana kutokuwa na abiria ndani halikadhalika idadi
kubwa ya mabasi yakibakia ndani ya kituo hicho.
Kufuatia mgomo huo uliotikisa nchi kutokana na mamia ya wasafiri
kukwama maeneo mbalimbali ya nchi huku abiria wanaotumia usafiri wa
daladala wakilazimika kutembea kwa miguu baadhi ya viongozi wa vyama vya
siasa wamefika kituo kikuu cha mabasi ubungo na kuzungumza na abiria
pamoja na madereva hao akiwemo Mwenyekiti chadema Freeman Mbowe na Prof
Ibrahim Lipumba Mwenyekiti CUF nahivyo shughuli kuanza na dala dala
kufanya safari zao kama kawaida.
Via>>ITV
Social Plugin