Takriban watu 430 wamekufa kutokana na wimbi la joto linalovuma nchini India.
Watafiti wamesajili kiwango cha juu mno cha nyuzi joto 48'C katika maeneo mengi nchini humo.
Vifo
vingi zaidi vimeripotiwa katika majimbo ya kusini ya Telangana na
Andhra Pradesh, ambapo watu 140 wamepoteza maisha yao kuanzia jumamosi
wimbi hilo la joto lilipotokea.
Mji wa Allahabad ulioko Uttar
Pradesh ulisajili vipimo vya nyuzi joto 48C huku wakazi wa mji mkuu wa
India New Delhi ukistahimili kiwango cha nyuzi joto 44C .
Maafisa wa utawala nchini humo wameanza kampeni ya kuwahamasisha
wananchi kukaa majumbani mwao na kuwashauri wanywe waji mengi.
Yamkini
viwango vya joto vimekuwa juu zaidi katika kipindi cha mwezi mmoja
uliopita lakini vifo vimeanza kuripotiwa mwishoni mwa juma.
Jimbo
la Andhra Pradesh ndilo lililopoteza watu wengi zaidi ikiwa na jumla ya
watu 246 waliopoteza maisha yao kuanzia juma lililopita.
"asilimia kubwa ya wale waliopoteza maisha ni watu wenye umri wa
zaidi ya miaka 50 walioshinda nje ya majumba yao.'' alisema kamishna wa
kupambana na majanga katika jimbo la Andhra Pradesh.
Waaandishi wa habari wanasema kuwa watu 186 wameaga dunia katika wilaya 10 za jimbo la Telangana.
Watu 58 wamekufa kuanzia siku ya Jumamosi.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa imesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa hali hiyo ya joto kuendelea kwa siku kadhaa zijazo.
Watu wengine kumi walipoteza maisha yao katika jimbo la Magharibi mwa Bengal.
Waendesha
teksi ambazo hazina kiyoyozi hawataruhusiwa kuhudumu kwa saa tano
katika mji mkuu wa Kolkata. Hii inafuatia vifo vya madereva wawili.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa inasema kuwa hali hiyo ya juu ya joto inatokana na ukosefu wa mvua.
Via>>BBC
Social Plugin