Mtoto mmoja wa miaka minane
amesafirishwa hadi nchini Uhispania kutoka Morroco akiwa ndani ya
sanduku kwa mujibu wa maafisa wa polisi wa Uhispania.
Mvulana huyo
kwa jina Abou alipatikana ndani ya sanduku hilo lililokuwa limebebwa na
msichana wa miaka 19 kuelekea Cueta,eneo lililo karibu na taifa la
Morocco siku ya Alhamisi.
Wakati polisi walipolifungua sanduku
hilo, mvulana huyo alikuwa katika hali mbaya sana.
Mvulana huyo kutoka
Ivory Coast sasa anahudumiwa na mamlaka ya Cueta.
Gazeti la
Uhispania El Paris liliripoti kwamba msichana huyo wa miaka 19 hana
uhusiano na mtoto huyo na kwamba alilipwa na babaake ili kubeba sanduku
hilo.
Babaake mtoto huyo anaishi katika visiwa vya Conary na kwamba alitarajia kuonana na mwanawe kulingana na gazeti hilo.
Chombo cha habari cha Uhispania Efe kimesema kuwa babaake mvulana
huyo ambaye anajulikana kama Abou alisafiri hadi nchini Ivory Coast
kumchukua mwanawe baada ya kuhamia katika eneo la Gran Canaria mwaka
2013.
Babaake baadaye aliripotiwa kumlipa raia huyo wa Morocco ambaye alimsafirisha mtoto huyo kupitia sanduku.
Msemaji wa polisi aliiambia Efe:''Alionekana kusita na kama ambaye hakutaka kupitia mpakani''.
Via>>BBC
Social Plugin