Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwenyekiti wa mtaa wa Ndembezi
katika manispaa ya Shinyanga Jumanne Maziku amevunjika mguu wa kushoto baada ya
kupigwa tofali baada ya kukutwa akijisaidia haja ndogo kwenye ukuta wa nyumba ya
mtu iliyopo karibu na baa.
Tukio hilo limetokea usiku wa kumkia leo katika eneo la Ngokolo
Mitumbani mjini Shinyanga baada ya
mwenyekiti huyo kudaiwa kujisaidia kwenye ukuta wa nyumba ya mwanamke mmoja
mkazi wa Ngokolo.
Akizungumza na Malunde1 blog akiwa kwenye hospitali ya mkoa
wa Shinyanga akisubiri rufaa ya kwenda hospitali ya Bugando jijini Mwanza
mwenyekiti huyo amesema haya:>>
“Ilikuwa majira ya saa mbili,nikiwa na wenzangu tukinywa
pombe,ghafla nikapigiwa simu na mtu nikainuka,hapo kuna mti na mazingira ya
vichaka vichaka,nikaanza kuzungumza na simu baadaye nikaanza kujisaidia”>Jumanne Maziku.
“Wakati
naendelea kujisaidia,akaja jamaa mmoja akaniuliza,kwanini unajisaidia
hapa?,mimi sikumsemesha,nikaanza kurudi kwa wenzangu pale kwenye grocery ghafla
nikaanza kupigwa,huenda aliyenipiga ni kijana wake na mama mwenye nyumba,sasa
hivi ndiyo anasimamia matibabu yangu”>Maziku
Maziku amesema kitendo
alichofanyiwa ni udhalilishaji kwake kwa sababu hakuwa najisaidia katika nyumba
hiyo.
Naye mama mwenye nyumba alikokutwa anakojoa amesema
ameambiwa atoe shilingi laki 7 kwa ajili ya matibabu ya mwenyekiti huyo wa mtaa
aliyepigwa tofali.
Hata hivyo wa bar alikokuwa anakunywa pombe bi Halima Kisena
amesema kitendo cha mwenyekiti wa mtaa kupigwa tofali kinatokana na ulevi wake
na si kukosekana kwa vyoo katika baa zake.
“Katika bar zangu zote kuna vyoo,sijui kilichompeleka huko
na kujisaidia kwenye ukuta wa watu,ulevi wake ndiyo umemponza”,amesema Kisena.
Na Mwandishi maalum wa Malunde1 blog Shinyanga
Social Plugin