Askari
Polisi saba akiwemo mkuu wa kituo cha Polisi Murongo wilaya ya Kyerwa
mkoani Kagera Bw.Richard Msusi wanatuhumiwa kupora fedha zaidi ya
shilingi milioni saba baada ya kuwateka nyara maafisa wa halmashauri ya
wilaya ya Kyerwa wakitumia bunduki na mabomu eneo la Murongo katika
mpaka wa Tanzania na Uganda wakigombea kukagua gari lenye shehena ya
bidhaa ambazo haziruhusiwi kuingia hapa nchini.
Maafisa wa halmashauriya wilaya ya Kyerwa baada
ya kuachiwa huru na jeshi la polisi wamesema kuwa chanzo cha kukamatwa
na kuporwa fedha ni baada ya kuwazuia Polisi wasiruhusu gari lenye
shehena ya bidhaa zisizoruhusiwa kuingia hapa nchini zikiwemo pombe
haramu aina ya Empire zinazozalishwa nchi ya Uganda kwa madai kuwa gari
hilo limekaguliwa na maafisa wa TRA na polisi kwenye mpaka wa Tanzania
na Uganda hivyo halmashauri haina mamlaka ya kukagua gari hilo hali
iliyosababisha mgogoro kati ya polisi na maafisa wa halmashauri.
Kufuatia hali hiyo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye
ni mkuu wa mkoa wa Kagera Bw.John Mongella akalazimika kwenda katika
eneo la tukio ambapo akiwa njiani katika hali isiyokuwa ya kawaida
barabara ya kaisho Murongo ikafungwa na vifusi vya mchanga hali
iliyosababisha polisi kumsimamia mkandarasi kusambaza vifusi vya mchanga
ili kuruhusu msafara wa mkuu wa mkoa upite ambapo katibu wa CCM wilaya
ya Kyerwa Bi.Odilia Maholelo ameshangazwa na kitendo cha kufungwa
barabara inayotumika.
Baada ya barabara kufunguka msafara ukaendelea ambapo mkuu wa mkoa
wa Kagera Bw.John Mongella akaitisha kikao cha kamati ya ulinzi na
usalama wilaya ya Kyerwa na baadaye akazungumza na ITV akisema kwamba
ofisi yake inachunguza kwa kina tuhuma hizo na atakayebainika kukiuka
sheria za tumishi wa umma atawajibishwa kisheria.
Via>>ITV
Social Plugin