Nchi ya Ivory Coast imepiga marufuku uigizwaji uuzaji na usambazaji wa bidhaa zozote zenye uwezo wa kuchubua rangi ya ngozi ya binadamu .
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Wizara ya afya imetangaza kuwa ni haramu kuingiza bidhaa hizo katika namna yeyote iwe ni vipodozi ama matembe kwa sababu ya athari zake kwa afya.
Bidhaa nyingi za kijichubua rangi ya ngozi zinauzwa katika taifa hilo la Magharibi mwa Afrika.
Marufuku
hiyo inaharamisha uingizwaji wa vipodozi ,mafuta, na tembe zenye madini
ya zebaki na vyuma vinavyotumiwa kuchubua rangi pamoja na kemikali
zingine nyinginezo.
Mwanamke aliyetumia ''Mkorogo''
Kulingana na afisa wa halmashauri inayosimamia matumizi ya madawa nchini humo Christian Doudouko,
Idadi
ya watu ambao sasa wanaonesha za kuathirika kiafya na madawa
hayo ya kuchubua ngozi imeongezeka mno katika miaka ya hivi punde na
kulazimisha wizara ya afya kuchukua hatua hiyo kali.
Afisa huyo aidha alisema kuwa madini hayo haswa Zebaki yanaweza kusababisha maradhi ya saratani ya ngozi.
Daktari Elidje Ekra alisema kuwa kemikali zinazotumika ilikuhakikisha ufanisi wa kuchubua rangi asili ya binadamu zinachangia pakubwa kuzuka kwa matatizo ya shinikizo la damu pamoja na hata Kisukari.
Daktari Elidje Ekra alisema kuwa kemikali zinazotumika ilikuhakikisha ufanisi wa kuchubua rangi asili ya binadamu zinachangia pakubwa kuzuka kwa matatizo ya shinikizo la damu pamoja na hata Kisukari.
Daktari
Ekra ambaye ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Treichville Abidjan anasema
ameshuhudia magonjwa mengi tu ya ngozi yasiyo na tiba na kila alipofanya
upelelezi aligundua kuwa wagonjwa walikuwa pia ni watumizi wa mikorogo.
Mikorogo
hiyo ya kujichubua ngiozi na maarufu mno katika mataifa mengi ya Afrika
huku wanawake wengi wakipendelea kujichubua iliwakubaliwe kuwa ni
warembo.
Senegal imeanza kampeini ya kupinga ''mikorogo''
Senegal imeanza kampeini ya kupinga ''mikorogo''
Kasumba hiyo ikichochewa na dhana kuwa mwanamke mrembo sharti awe na ngozi laini na nyeupe.
Matumizi ya mikorogo sasa hata imeanza kupata umaarufu miongoni mwa wanaume.
Licha
ya kutokuwepo na takwimu maalum kuhusu matumizi ya mikorogo hiyo,
mabango ya mauzo na kunadi bidhaa zenye uwezo wa kukufanya uwe
''Mrembo'' zimezagaa kote barani Afrika.
Haijajulikana hadi sasa wanawake wanaozitumia wamelichukulia vipi kauli hiyo ya serikali.
Social Plugin