STAA
wa filamu Bongo, Kajala Masanja, kupitia akaunti yake ya Instagram hivi
punde amesema maisha yanaendelea ikiwa ni siku mbili baada ya kupigwa
chupa na mtu asiyemfahamu usiku wa kuamkia Jumatatu akiwa klabu wakati
alipokwenda katika shoo ya kumchangia mke wa Mabeste, Maisha Club
Kajala alieleza kuwa tukio hilo lilitokea wakati akijiandaa kutoka Maisha Club ambapo ghafla akiwa kwenye ngazi alirushiwa chupa kichwani iliyopelekea kuanguka kutoka kwenye ngazi hadi chini na kusaidiwa na wasamaria wema waliompeleka Hospitali ya Mwananyamala ambapo alishonwa kwenye jeraha alilolipata.
Staa huyo aliongeza kuwa mtu aliyempiga chupa ni mwanaume na tayari yupo mikononi mwa polisi japo kabla ya tukio hilo alikuwa hamjui na wala hajawahi kumuona mtu huyo.

Social Plugin