Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUHUSU STAA WA FILAMU BONGO KUPIGWA CHUPA USIKU AKIWA KLABU

STAA wa filamu Bongo, Kajala Masanja, kupitia akaunti yake ya Instagram hivi punde amesema maisha yanaendelea ikiwa ni siku mbili baada ya kupigwa chupa na mtu asiyemfahamu usiku wa kuamkia Jumatatu akiwa klabu wakati alipokwenda katika shoo ya kumchangia mke wa Mabeste, Maisha Club

Kajala alieleza kuwa tukio hilo lilitokea wakati akijiandaa kutoka Maisha Club ambapo ghafla akiwa kwenye ngazi alirushiwa chupa kichwani iliyopelekea kuanguka kutoka kwenye ngazi hadi chini na kusaidiwa na wasamaria wema waliompeleka Hospitali ya Mwananyamala ambapo alishonwa kwenye jeraha alilolipata.

Staa huyo aliongeza kuwa mtu aliyempiga chupa ni mwanaume na tayari yupo mikononi mwa polisi japo kabla ya tukio hilo alikuwa  hamjui na wala hajawahi kumuona mtu huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com