Idhaa ya kiswahili ya BBC
imethibitisha kuwa taarifa tuliyochapisha kwamba kuna mgahawa mmoja
nchini Nigeria unaouza nyama ya binadamu sio za kweli.
Tunaomba radhi kwa taharuki au hisia zozote zilizosababishwa na taarifa hiyo.
Tunazingatia
kwa thamani kubwa sifa ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC kama Idhaa
inayozingatia uhakika wa habari zake na msimamo wa kutoegemea upande
wowote na ni kwa sababu hiyo tunachukua hatua stahiki kuhakikisha kosa
kama hilo halifanyiki tena.
Tunaomba radhi kutokana na taarifa
ambayo tuliichapisha hapa kuhusu mkahawa mmoja nchini Nigeria.Taarifa
hiyo haikuwa sahihi na ilichapishwa bila kuzingatia utaratibu wa BBC.
Tumeiondoa taarifa hiyo kwenye mtandao na tayari tumeanza uchunguzi
kuthibitisha ni nini kilichosababisha taarifa kama hiyo kuchapishwa.
Chanzo-BBC
Social Plugin