Moja ya story kubwa kuripotiwa na kituo
cha ITV jioni hii ni ishu ya watoto watatu wa kiume kukutwa wakiwa
wamejificha kwenye chasis ya basi.
Watoto hao wamekutwa Singida ambapo tayari walikuwa wamesafiri kutoka Kahama na walikuwa wakielekea Arusha.
Watoto hao wamesema walitolewa na mtu
mmoja Arusha kwenda Kahama akawaambia kuna kazi, walipofika Kahama
akawatelekeza, baadae wakaamua kurudi kwa njia hiyo ya kujificha kwenye
chasis ya basi.
Kamanda wa Polisi Singida ACP Thobias Sedoyeka amesema watoto hao walikutwa wakati wakaguzi wa mabasi walipokuwa wakikagua basi hilo la Mgamba Express ambapo mpaka wanafika hapo basi lilikuwa limesafiri kwa zaidi ya Kilometa 360.
Habari yote iko hapa chini sikiliza sauti
Social Plugin