Dubai ni
moja kati ya miji inayokua kwa kasi sana duniani. Na ni miongoni mwa
miji ambayo inafahamika kwa majengo ya kipekee na kifahari huku watu
wengi kutoka sehemu mbali mbali duniani wakivutiwa kwenda Dubai kutalii ama kufanya biashara.
Kwenye headlines leo ni mpango wa
kuboresha michezo nchini humo, ambapo unaambiwa wameaamua kujenga uwanja
wa kisasa wa mchezo tennis chini ya bahari.
Dubai wako kwenye mkakati wa kutekeleza project yao mpya unaojulikana Underwater Tennis Stadium itakayowezesha mashabiki wa mchezo wa tennis Dubai na duniani kuenjoy kucheza au kushuhudia mechi za tennis chini ya maji.
Krzysztof Kotala ndio
msanifu majengo mkuu anaehusika na ujenzi wa uwanja huo wa chini ya
maji na anasema anataka uwanja uwe zaidi ya uwanja wa michezo kwani
utakuwa na sehemu ya vivutio vya kitalii kwa watu wanaopenda kwenda Dubai kwa matembezi yao binafsi.