Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwasili jijini Arusha kuongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Patandi.
Waziri Mkuu Mstaafu Edward
Lowassa akilakiwa na baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislamu jijini
Arusha alipowasili kwa ajili ya kuongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa
msikiti wa Patandi. Waziri mkuu wa zamani Edward Lowasa ameendesha harambee na kuchangisha zaidi ya milion mia mbili kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya kiislam inayojengwa mkoani Arusha.
Katika harambee hiyo Lowasa ambaye alipata mapokezi makubwa
kutoka kwa wananchi na viongozi wa mkoa wa Arusha aliwasilisha mchango
wa milioni mia moja na tano zilizojumuisha mchango wake mwenyewe na
wadau wadau mbali mbali akiwemo makamu wa rais Dr. Mohamed Gharib Bilal
aliyemwakilisha.
Akizungumza katika harambee hiyo Sheikh mkuu wa mkoa wa Arusha Shaban
Bin Jumaa pamoja na kuwashukuru wote waliojitolea amewataka watanzania
kuendelea kuonyesha umoja wao kwa vitendo kwa kusaidiana bila kuongiza
itikadi zao za kidini na za kisiasa.
Katibu wa Bakwata mkoa wa Arusha Bw Abdalah Masoud amesema shule hiyo
ya sekondari ya kiislam inayojengwa katika eneo la Tengeru wilayani
Arumeru inatarajiwa kugharimu zaidi ya bilioni moja itakapokamilika na
itasomesha watoto wote bila kujali itikadi zao.
Harambee hiyo ilihudhuriwa na wananchi na viongozi wa kada
mbalimbali, wakiwemo wa kisiasa, wafanyabiashara wakubwa wakiwemo wa
madini, na vijana wanaoendesha pikipiki maarufu kama bodaboda.
Via>>ITV
Social Plugin