Moja ya story kubwa kwenye siasa za Tanzania
wiki iliyopita ilikuwa ishu ya CCM kuwafungulia makada wake sita ambao
walikiuka kanuni za chama hicho kwa kutangaza kugombea Urais mapema
kinyume na utaratibu wa chama hicho, mmoja ya waliokuwa wamefungiwa ni
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa.
Jana kulikuwa na stori ya Naibu Waziri Mwigulu Nchemba kutangaza kugombea Urais wa Tanzania kupitia CCM.. leo Mbunge Edward Lowassa
ameongea kuhusu mambo kadhaa ikiwemo hali ya afya yake, chuki kwenye
siasa, na ujumbe wake kwa CCM kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 Tanzania.
Waziri
Mkuu mstaafu Edward Lowassa leo amefanya mkutano maalum nyumbani
kwake mjini Dodoma na wahariri wakuu wa vyombo mbalimbali vya
habari hapa nchini.Katika
mkutano huo ameambatana na Nazir Karamagi, Peter Serukamba, Diana chilolo, Hussein Bashe na wengineo . Katika mkutano huo kwa ufupi Lowassa amesema
yafuatayo;
"Kuhama
chama sina mpango.. nimeingia CCM toka 1977 sijafanya kazi mahali
pengine popote isipokuwa CCM.. My life is CCM.. huyo ambae hanitaki CCM
ndio ahame sio mimi nihame" Edward Lowassa.
1. Amesema Hahusiki lolote na sakata la Richmond na ndio sababu hata kamati ya Mwakyembe haikuona sababu ya kumhoji.
Amesisitiza kuwa cheo cha uwaziri mkuu ndio ilikuwa lengo la kamati ya Mwakyembe na spika wa bunge kipindi hicho Samwel Sitta.
Amesisitiza hicho sio kikwazo kwake katika kuingia Ikulu kwani sakata la Richmond lilipikwa kumchafua. Amechukua muda mrefu kuzungumzia hili la Richmond na amesema atalisema zaidi Arusha wikendi hii.(Jumamosi)
Amesisitiza kuwa cheo cha uwaziri mkuu ndio ilikuwa lengo la kamati ya Mwakyembe na spika wa bunge kipindi hicho Samwel Sitta.
Amesisitiza hicho sio kikwazo kwake katika kuingia Ikulu kwani sakata la Richmond lilipikwa kumchafua. Amechukua muda mrefu kuzungumzia hili la Richmond na amesema atalisema zaidi Arusha wikendi hii.(Jumamosi)
2.
Anaamini kila mtangaza nia ana makundi ya kumuunga mkono.
3.
Lengo kuu atakaloanza nalo ni Elimu na sio Kilimo kwanza .Amesema
serikali ya JK ilikosea kuanza na kilimo na kuweka kando elimu.
Ametangaza kuwa sera yake ni Elimu Kwanza."Tukiwekeza vizuri katika elimu tunaweza kubadilisha nchi yetu.. Tukitaka kuokoa nchi yetu tuwekeze kwenye elimu"-Lowassa.
4.
Kuhusu pesa anasema anapata michango ya rafiki zake na ataendelea
kupokea michango hii wakati wote wa harakati zake na haina madhara
yotote.
5.
Anasema hatahama CCM na asiyemtaka yeye CCM ndiye aondoke ndani ya chama
kwani yeye ana uhakika wa kupata nafasi kuwania urais.
6. Amesema hatalipa kisasi kwa lolote lililomtokea katika siasa. Amemwachia Mungu kwani yeye ni mcha Mungu.
“Mimi ni Mkristo, ninaamini kwenye dini yangu sana… sina kisasi na mtu yoyote“>>>Lowassa
7."Kuna
chuki imeibuka kwenye siasa za nchi yetu na kutakiana mabaya, afya ni
neema kutoka kwa Mungu.. mimi niko sawa kabisa kwa chochote kile..
kwenye Chama chetu waweke utaratibu tukapimwe wote afya mimi nitakuwa wa
kwanza kwenda kupima tuelezane nani mgonjwa"-Lowassa.
8.
Amesema Arusha itawaka moto tarehe 30 mwezi huu na kuwataka watanzania
kutega sikio kwani ataanika kila jambo kuhusu mustakabali wa nchi hii na
mipango yake ya kuiinua nchi kiuchumi katika miaka kumi ijayo.
9.Sentensi yake nyingine kuhusu tatizo la ajira>>>”Tatizo
la ajira ni bomu lisiposhughulikiwa.. toka nimetoka Serikalini kuna
vitu ambavyo kama tungevifanya kwa kasi ile ambayo tulianza nayo
ningepita napunga mkono nikapata kura zote, hatufanyi maamuzi iwe magumu
au rahisi.. mambo yanakwenda legelege, Rais amefanya jitihada kubwa
sana lakini kuna mambo hayaendi>>> Edward Lowassa.
10.“Upinzani
umeanza kupata nguvu kubwa sisi ni chama dola tusibweteke.. wenzetu
wanajiandaa vizuri na sisi tujiandae vizuri. Tusifanye mchezo
tusibweteke”>>> Mbunge Edward Lowassa.
Kwa dakika tatu kayazungumza haya, sauti yake unaweza kuisikiliza hapa kwa kubonyeza play !!