Siku
moja baada ya mgomo wa madereva kumalizika madereva 15 wa daladala na
mabasi makubwa wamesimamishwa kazi na wamiliki wa mabasi hayo kwa madai
ya kujihusisha na mgomo huo.
Katibu wa chama cha madereva Rashid Salehe ametoa taarifa hiyo
jijini Dar es salaam ambapo amesema madereva 18 wamefikishwa mahakamani
huko mkoani Dodoma na kuongeza kuwa endapo wangekuwa na mikataba
wanayopigania hivi sasa wasingefukuzwa kazi kienyeji namna hiyo.
Akizungumzia kamati iliyoundwa na serikali kushughulikia suala hilo
baada ya mkuu wa wilaya ya kinondoni kuwaahidi kuwa ile iliyoundwa na
waziri mkuu itafanyiwa maboresho wamesema hawana imani nayo baada ya
idadi ya wamiliki ambao ndiyo wanaowalalamikia kuwa kubwa zaidi yao.
Madereva hao wana madai ya msingi matano ambayo ni pamoja na
mikataba bora ya kazi, faini za mara kwa mara hata kwa kosa linalohitaji
onyo, ukaguzi uliopitiliza, kwenda kusoma kila baada ya leseni kuisha
muda wake na mwendo wa kilomita 80 kwa saa madai yaliyosababisha mgomo
uliotikisa nchi.
Via>>ITV
Via>>ITV
Social Plugin