Polisi
jijini Dar wamewakamata watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa katika
jaribio la kuiba pesa katika benki ya NMB iliyopo Sinza-Mori, Dar es salaam.
Tukio
hilo limetokea mchana wa leo katika Benki ya NMB tawi la Sinza-Mori
jijini Dar ambapo majambazi hao walikamatwa wakiwa katika harakati za
kutekeleza tukio hilo.
Majambazi hao baada ya kukamatwa wamepelekwa katika kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Wananchi wakiwa eneo la Benki ya NMB Sinza-Mori, Dar wakifuatilia tukio hilo.
Gari walimowekwa majambazi hao wakati wakipelekwa kituo cha Polisi Mabatini, Kijitonyama.
Social Plugin