Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAJAMBAZI YAKAMATWA YAKIJIANDAA KUIBA PESA BENKI YA NMB


Majambazi hao wakiwa wametiwa pingu baada ya kukamatwa na jeshi la Polisi jijini Dar es salaam.
 
Polisi jijini Dar wamewakamata watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa katika jaribio la kuiba pesa katika benki ya NMB iliyopo Sinza-Mori, Dar es salaam.
Tukio hilo limetokea mchana wa leo katika Benki ya NMB tawi la Sinza-Mori jijini Dar ambapo majambazi hao walikamatwa wakiwa katika harakati za kutekeleza tukio hilo.

Majambazi hao baada ya kukamatwa wamepelekwa katika kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama jijini Dar es salaam.




Wananchi wakiwa eneo la Benki ya NMB Sinza-Mori, Dar wakifuatilia tukio hilo.
Gari walimowekwa majambazi hao wakati wakipelekwa kituo cha Polisi Mabatini, Kijitonyama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com