Wananchi
wa kijiji cha Nduoni kata ya Kirua magharibi wilaya ya Moshi mkoani
Kilimanjaro wamelazimika kuvunja ofisi ya afisa mtendaji wa kijiji
ambayo imefungwa kwa zaidi ya miezi sita kutokana na vurugu za kumkataa
mwenyekiti aliyeapishwa kwa makosa katika uchaguzi mdogo wa serikali za
mitaa uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
Wananchi hao wamelazmika kuvunja ofisi hiyo na kumuingiza
mwenyekiti aliyeshinda kihalali katika uchaguzi huo Bw.Thomas Ngowi na
afisa mtendaji Camilus kessy kwa madai ya kukosa huduma muhimu kwa muda
mrefu na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya kijiji hicho.
Wamesema kukosekana kwa uongozi wa kijiji hicho kumesababisha
miradi ya maendeleo kukwama sanjari na wananchi kulazimika kwenda katika
kijiji cha jirani kutafuta huduma.
Akizungumza mara baada ya kufunguliwa kwa ofisi hiyo mwenyekiti wa
kijiji hicho Bw.Thomas Ngowi amesema zaidi ya wananchi wapatao 2800
wamekuwa wakitaabika kwa kukosa hudumaa katika kijiji hicho na kwamba
yuko tayari kufanyakazi kwa kushirikiana na mtendaji wa kijiji hicho kwa
lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.
Naye afisa mtendaji wa kijiji cha Nduoni Bw.Camilius Kessy amesema
mweneykiti huyo ndiye aliyechaguliwa na wananchi kihalali na kuahidi
kushirikiana naye pamoja na wananchi wa kijiji hicho ili kutoa huduma
bora za kuleta maendeleo katika kijiji hicho.
Via>>ITV
Social Plugin