Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Makubwa Haya!! MWANAMKE AMEWAPIGA BUSU HOVYO WANAUME KIBAO,KILICHOFUATA NI UMAARUFU ULIOPITILIZA

 

Wanachuo wa chuo kikuu cha Wellesley ,nchini Marekani wana utamaduni wa kuwapiga busu wafukuza upepo wa mbio za Boston Marathon,utamaduni wa ambao ni wa zama za kale mno,lakini safari hii si mwanafunzi bali mwanamke mmoja aliamua kujitoa muhanga na kuamua kutoa busu lililomgharimu kwa kubusu wanaume hovyo alipokuwa akishiriki katika mbio hizo mwezi uliopita.

Mwanariadha huyo Barbara Tatge,alimpata mwanamume aliyekuwa radhi kupigwa picha wakati akimbusu ,basi baada yam bio hizo mtoto wa mwanamke huyo aliamua kumsaka mwanamume huyo mitandaoni.picha hiyo ya busu ikasambaa ulimwenguni,na kusababisha mke wa mwanamume huyo kumtumia barua.

Akimwambia yeye hajachukia kwa kitendo chao cha kubusiana.

 Nakuhakikishia amini hivyo, hata marafiki zetu pia wamejipatia umaarufu mkubwa kupitia kitendo chenu hicho hasa tukisikia habari mnamsaka mume wangu,binafsi nilivutiwa na kitendo hicho ,hata hivyo nakutia moyo kushiriki tena safari ijayo na pia nakutakia mbio njema wakati ujao.hongera kwa kumaliza mbio hizo Boston!” imemaliza barua hiyo.

Mwanariadha huyo Tatge baada ya kuupokea waraka huo akajiapiza kutowabusu tena waume za watu wakati ujao. 
Na baada ya hapo mama huyo alimshukuru mwanawe kwa kujitolea na kuutangaza utamadunia wa Wellesley na katika siku za usoni mwanamke huyo atawabusu wanaume ambao hawajaoa tu.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com