TZ kuna matukio ambayo yamewahi kusikika
kuhusu wanawake wanaovaa nguo fupi kuchaniwa nguo zao, Kenya pia hiyo
iliwahi kukaa kwenye headlines.
Kwa nchi za wenzetu si jambo la ajabu
kuona wanawake wakiwa ndani ya mavazi mafupi na kutembea bila wasiwasi
barabarani, mna leo kuna hii ya uvaaji wa nguo fupi iliyotokea China.
Kuna mgahawa mmoja China umejitolea kuwapa punguzo wanawake wote watakaokuwa wamevaa nguo fupi wanapoingia ndani ya Mgawaha huo.
Kuonesha jamaa wako serious kabisa
amewekwa na mtu maalum kabisa kwa ajili ya kupima ufupi wa nguo ya kila
mwanamke anayeingia kwenye mgahawa huo.. hii imeonekana kupata wateja
wengi, jamaa wanasema muda mwingi kuna foleni ndefu ya wateja wa kike
ambao wanapiga sketi zao ili kuingia ndani.
Punguzo hilo huanzia asilimia 20 hadi 90 ya gharama ya chakula na vinywaji na hutegemea na jinsi mhusika alivyovaa.
Yang Jia Hot Pot
ambaye ni meneja wa mgahawa huo amesema baada ya kutoa ofa hiyo
wamekuwa wakipata idadi kubwa ya wateja na mauzo yamekuwa poa pia baada
ya kuanza kwa ofa hii maalum kabisa !!
Social Plugin