Tatizo
la unywaji pombe wa kupindukia kwa wanaume wilayani hapa, limechukua
sura mpya baada ya jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro kutuhumiwa
kushiriki kuchochea biashara hiyo.
Akiongea katika mkutano wa hadhara kuhusu tatizo hilo, Mkuu wa Mkoa
wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, alisema kuwa taarifa mbali mbali
zinaonyesha kuwa baadhi ya askari si waaminifu katika vita dhidi ya
pombe haramu inayoendelea hivi sasa wilayani humo.
“OCD taarifa zinaonyesha kuna baadhi ya askari wako, ambao
wanashirikiana na wafanyabiashara wa pombe haramu ya gongo na hili
linafanya kazi ya operesheni kukomesha tabia hii mbaya kuwa ngumu,”
alisema.
Alisema taarifa hizo zikiwamo zile za kutoka kwa wananchi wenye nia njema na vita hiyo, zinaonyesha kuwa baadhi ya askari wasio waaminifu wamewageuza wafanyabiashara wa gongo kuwa ATM zao (mashine za kutolea pesa) kwa kuchukua rushwa hivyo kusababisha uovu huo uendelee.
Alisema taarifa hizo zikiwamo zile za kutoka kwa wananchi wenye nia njema na vita hiyo, zinaonyesha kuwa baadhi ya askari wasio waaminifu wamewageuza wafanyabiashara wa gongo kuwa ATM zao (mashine za kutolea pesa) kwa kuchukua rushwa hivyo kusababisha uovu huo uendelee.
Gama alisema serikali haijamzuia mtu kunywa pombe halali ili mradi
isiwe ni wakati wa kazi na kwamba pale itakapobainika kuna wanao kunywa
wakati wa saa za kazi watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.
“Inasikitisha kusikia kuwa baadhi ya pombe zinazonyweka Rombo
zimetengenezwa na mbolea aina ya urea, maji ya betri, spiriti, kinyesi
cha binadamu, sukari guru na molasesi, hii ni hatari kwa afya ya
mwanadamu,” alisema.
Kwa upande wake Padri Serafini Kilawe, wa Kanisa Katoliki, alisema
kuwa vita dhidi ya pombe haramu hasa ya gongo haitaweza kumalizika iwapo
baadhi ya askari hawataacha kushirikiana na wanaotengeneza pombe hizo.
Suala la ulevi uliokithiri limekuwa gumzo maeneo mbali mbali
mkoani Kilimanjaro na nje ya mkoa huo, ambapo imedaiwa kuwa baadhi ya
wanawake wilayani humo wanalazimika kukodi wanaume kutoka nchi jirani ya
Kenya ili kukidhi mahitaji yao ya kindoa.
Wananchi waishio wilayani hapo, Elizabeth Shabani na Mary Shirima,
walikiri kuwapo kwa askari, wanaofika maeneo wanapotengenezea pombe
haramu kuchukua fedha kila mwisho wa mwezi kama ni ujira wa kuwalinda.
Via>> NIPASHE
Social Plugin