Jeshi
la Polisi Mkoani Mwanza linamshikilia bibi mmoja aitwaye Laurencia Athanas mkazi wa Kiseke, Ilemela jijini
Mwanza kwa tuhuma za kumchoma visu vya moto mjukuu wake na
kumsababishia majereha mbalimbali mwilini akimtuhumu kupoteza
peni (kalamu) ya shilingi 200.
Mtoto
huyo aitwaye Jackson Hosea ( 10 ) ambaye ni mwanafunzi wa
darasa la tatu katika shule ya msingi Kiseke iliyoko Ilemela
Jijini Mwanza alifanyiwa unyama huo nyumbani kwa bibi huyo
ambaye ni mzazi wa mama yake aishiye Nzega siku ya Ijumaa
jioni tarehe 23 Mei 2015.
Via>>Mpekuzi |
Social Plugin