Sio tukio la kawaida kukutana na mtu
kavaa gauni la harusi kwenye mazishi.. Lakini hii ya leo kali kutoka Kenya, kuna hii stori kutoka Kaunti ya Vihiga, unaambiwa
mwanamke aliyefiwa na mume wake akalazimishwa kuvaa gauni ambalo anavaa
bibi harusi wakati wa kufunga ndoa, alafu safari ya kwenda kwenye
mazishi ikaanza.
Mary Akatsa ni kiongozi wa Kanisa la Jerusalem Church of Christ
alikuwa akiongoza kila kitu mpaka mazishi yalipoisha, ukicheki kwenye
hii video huyo mama anaonekana mkali hivi kama unaenda tofauti na
maagizo yake.. wengine wanapigwa mpaka vibao.
Mazishi yalikuwa kama sherehe tu, kama
ukiiona hii video unaweza kuhisi labda watu walikuwa kwenye harusi au
sherehe nyingine ya kawaida.
Unaambiwa huu ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa waumini wote wa kanisa hilo, ikitokea mwanamke kafiwa na mume wake lazima avae shela la harusi siku ya mazishi ya mume wake.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
Unaambiwa huu ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa waumini wote wa kanisa hilo, ikitokea mwanamke kafiwa na mume wake lazima avae shela la harusi siku ya mazishi ya mume wake.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
Social Plugin