|
Maonesho ya
raha yake,wakati mwingine unaona vitu ambavyo hujawahi kuona tangu uzaliwe….basi
Malunde1 blog inakukutanisha na wataalam kutoka mgodi wa almasi wa Mwadui ( Williamson Diamonds Limited)
uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ambao wamekuja na Jiko la Kisasa
linatumia nguvu ya jua katika maonesho ya Viwanda Vidogo Kanda ya Ziwa
yanayoendelea katika Viwanja vya Shycom mjini Shinyanga.
|
|
Afisa Usalama,Afya na Mazingira kutoka mgodi wa Mwadui Donatus Mukungu akitoa maelezo juu ya mradi huo wa jiko la kutumia nguvu ya Jua kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga (mwenye miwani kushoto)aliyetembelea banda la mgodi huo Mei 30,2015. |
|
Afisa Mazingira kutoka Mgodi wa Mwadui Prisca John akionesha yai lililoiva ndani ya dakika 10 baada ya kuwekwa kwenye jiko hilo la kutumia nguvu ya jua |
Afisa Mazingira kutoka Mgodi wa Mwadui Prisca John akimenya yai
|
Afisa Usalama,Afya na Mazingira kutoka mgodi wa Mwadui Donatus Mukungu alisema majiko mengine ya namna hiyo yanaendelea kutengenezwa na wana mpanga wa kuanza kuyasambaza jijini |
|
Mfanyakazi kutoka Mgodi wa Mwadui akiwa amesimama mbele ya jiko hilo la kisasa |
|
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akiangalia asali iliyotengezwa katika mgodi wa Mwadui |
|
Afisa Usalama,Afya na Mazingira kutoka mgodi wa Mwadui Donatus Mukungu akieleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na mgodi wa Mwadui,ambapo alisema wanafanya kazi za kutunza mazingira pia |
|
Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika banda la mgodi wa Mwadui katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga |
|
Afisa Mazingira mgodi wa Mwadui(kushoto) akionesha nta iliyotengenezwa katika mgodi huo |
|
Afisa Mazingira mgodi wa Mwadui akiwaeleza wakazi wa Shinyanga namna shughuli za uchimbaji madini zinavyofanyika.
Maonesho ya 13 ya Viwanda Vidogo Kanda ya ziwa yameanza Mei
28 mwezi huu na Kilele chake kitakuwa Juni 2015 ambapo wajasiriamali mbalimbali
kutoka ndani na nje ya nchi wanaonesha kazi zao katika Viwanja vya Shycom mjini
Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com