Tarehe
27 na 30 Aprili, 2015, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI ilitangaza
ajira ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu na mafundi sanifu wa maabara
kwa kuweka orodha kwenye tovuti ya www.pmoralg.go.tz. Iliagizwa
kuwa waajiriwa wapya walipaswa kuripoti katika Mamlaka za Serikali
za Mitaa kuanzia tarehe 01 hadi 09 Mei, 2015.
Napenda
kuchukua nafasi hii kuutaarifu umma kuwa ofisi yangu ilipokea na
kuchambua maombi ya walimu ambao hawakuajiriwa awali; na walioomba
kubadilishiwa vituo kutokana na matatizo mbalimbali.
Vilevile
ofisi imezingatia kuwapanga tena walimu ambao kwa sababu za msingi
walishindwa kuripoti kufikia tarehe 09 Mei, 2015.
Walimu
wote waliopo katika orodha ya awamu ya pili wanapaswa kuripoti kuanzia
tarehe 01 hadi 05 Juni, 2015 kwenye ofisi za Wakurugenzi wa
Halmashauri kwa ajili ya kuajiriwa na kupangiwa vituo vya kazi.
Orodha ya walimu hao watakaoajiriwa katika halmashauri husika imegawanywa katika makundi yafuatayo:-
i. walimu wa cheti (Daraja IIIA) waliokosa ajira kwa awamu ya kwanza;
ii. walimu wa cheti (Daraja IIIA) waliobadilishiwa vituo;
iii. walimu wa masomo ya sanaa kwa ajili ya shule za sekondari ambao hawakupangiwa vituo;
iv. walimu waliobadilishiwa vituo wa masomo ya sanaa kwa ajili ya shule za sekondari;
v. walimu wa masomo ya sayansi na hisabati kwa ajili ya shule za sekondari ambao hawakupangiwa vituo; na
vi. walimu waliobadilishiwa vituo wa masomo ya sayansi na hisabati kwa ajili ya
shule za sekondari.
Utaratibu wa Ajira ya Walimu Awamu ya Pili
Kila
mwajiriwa mpya anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-i. kuwasilisha vyeti
halisi vya taaluma ya kuhitimu mafunzo ya ualimu, elimu ya sekondari,
cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake; na
ii.
atalipwa posho ya kujikimu kwa muda wa siku saba (7) na nauli ya
usafiri wa magari (ground travel), malipo hayo yatatolewa na halmashauri
husika.
Angalizo
i.
Walimu ambao wamekwisharipoti na mchakato wao wa ajira umeanza katika
Mamlaka za Serikali za Mitaa hawatahusika na mabadiliko haya hivyo
waendelee kufanya kazi katika halmashauri husika na hawahusiki na
upangaji wa awamu hii.
ii.
Walimu ambao walichelewa kuripoti tarehe 9 Mei, 2015 na majina yao
hayajaonekana katika mabadiliko haya wanatakiwa waende kuajiriwa katika
halmashauri walizopangwa awali (kwa kuzingatia orodha iliyotolewa kwenye
tovuti tarehe 30/4/2015). Aidha, walimu wa masomo ya sanaa ambao
hawakuripoti katika Halmashauri za Wilaya za Meru na Arusha
wamebadilishwa vituo.
iii.
Walimu waliopangwa ni wale wa masomo ya sanaa/biashara na cheti
waliohitimu mafunzo kwa mwaka wa masomo 2013/14 na wahitimu wa miaka ya
nyuma wa masomo ya sayansi na hisabati kwa ajili ya kufundisha katika
shule za sekondari.
iv.
Kituo cha kazi cha mwalimu ni shule na sio Makao Makuu ya Halmashauri,
posho italipwa baada ya mwalimu kuripoti na kuandika barua kupitia kwa
Mkuu wa Shule.
v.
Mwalimu hatapokelewa na kuaajiriwa kama ikitokea yupo katika orodha na
amehitimu shahada au stashahada zisizo za ualimu na wenye shahada za
ualimu zisizo na somo au masomo ya kufundishia katika shule za
sekondari.
vi. Ikibainika kuna mwalimu atakayekwenda kuripoti na kuchukua posho na kuondoka, atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.
Ni muhimu kuzingatia maelekezo haya, ikiwa ni pamoja na muda uliowekwa kuripoti kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.
Limetolewa na
Ndg. Jumanne A. Sagini
KATIBU MKUU
OFISI YA WAZIRI MKUU-TAMISEMI
______________
5.Orodha ya Walimu wa Sanaa(Shahada/Stashahada) Awamu ya Pili Waliopangiwa Vituo Vipya - 23 Mei 2015
********************************************************************