Mschana
Judith Chomile(15) amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa
Morogoro akikabiliwa na tuhuma za kumnyonga hadi kufa mtoto mwenye umri
wa miaka 9 mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Bernard Benderi ya mjini Morogoro.
Akisoma shitaka mbele ya hakimu mkazi Ivan Msaki, mwendesha
mashataka wa polisi Aminata Mazengo amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo
may 20 kinyume na kifungu namba 196 cha kanuni ya adhabu nahakutakiwa
kujibu lolote kutokana na kosa lenyewe na kuwa mtuhumiwa yuko chini ya
miaka 18 hivyo kuwakilishwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 10 mwaka huu itakapo tajwa tena mahakamani hapo .
Katika hali isiyo ya kawaida ndugu wa marehemu Edga Mafwere kwa
hasira amempiga ngumi mtuhumiwa muda mfupi baada ya kutoka mahakamani
mbele ya maafisa wa jeshi la polisi na ustawi wa jamii ambapo naye
alijikuta katika mikono ya jeshi la polisi na kufungwa pingu ambapo
anashikiliwa kwa mahojiano zaidi.
Akizungumza juu ya uhakika wa usalama wa mschana Judith Chomile ,afisa ustawi wa jamii manispaa ya Morogoro Jasmin Masenge amesema
msichana huyo atakuwa katika mikono salama chini ya uangalizi wa
kitengo cha ustawi wa jamii pamoja na jeshi la polisi kitengo cha dawati
la jinsia na watoto hadi kesi inayomkabili itakapotolewa hukumu.
Via>>ITV
Social Plugin