Chama
cha wamiliki wa vyombo vya habari nchini -MOAT kimeunda kamati maalum
ya kuwashawishi wabunge ili wasiupitishie mswaada wa vyombo vya habari
kuwa sheria, baada ya kubaini kuwa unakusudia kufinya uhuru wa vyombo
vya habari, uhuru wa wananchi kupata habari na utaua vyombo vya habari
vya binafsi.
Maamuzi ya kuunda kamati hiyo yametolewa jijini Dar es Salaam baada
ya wamiliki wa vyombo vya habari nchini kukutana na kupata ufafanuzi wa
kisheria kuhusu muswada huo kutoka kwa mwanasheria wao Bw. Godfrey
Mpandikizi.
Akizungumza mwenyekiti wa MOAT Dr Reginald Mengi amesema Tanzania
inasifika duniani kwa amani, uwazi, na kwa kuwa na uhuru wa vyombo vya
habari, lakini sifa hizo zinaweza kufutika kama muswada huo utapitishwa,
hususan wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu.
Kabla ya kutoa maazimio hayo baadhi ya wanachama walitopata fursa
ya kuchangia mawazo walisema muswada huo wa sheria una nia mbaya kwa
tasnia ya habari na ni kinyume cha katiba ya nchi.
Katika hatua nyingine wakati
wizara ya mawasiliano Sayansi na Teknoljia ikiwasilisha bajeti ya
wizara yake bungeni mjini Dodoma, baadhi ya wabunge wamepinga vikali sheria mbalimbali ambazo
serikali imezipitisha ikiwemo ya miamala ya kieletoniki ya mwaka 2015 na
sheria nya udhibiti wa uhalifu wa mtandao wa mwaka 2015 kuwa inafifisha
uhuru wa watu kutoa taarifa mbalimbali ambazo zingeweza kusaidia
kuharakisha maendeleo katika nchi.
Akiwasilisha bajeti ya wizara yake Mh Profesa Makame Mbarawa
amesema wizara yake itahakikisha inaendelea kusimamia kwa kina sheria
zilizopo ili kuona kuwa tekinolojia haitumiki vibaya.
Akizungumza kuhusu sheria hizo Mh Mchungaji Peter Msigwa amesema
inashangaza kuona ni katika kipindi muhimu kama hiki ambacho watu
wanahitaji kupata taarifa nyingi tena za uhakika alafu serikali inabinya
uhuru wa wawatu kupata taarifa hizo.
Awali waziri wa viwanda na biashara Mh Abdallah Kigoda akiwasilisha
bajeti ya wizaya yake amesema serikali inakusudia kutoa leseni kwa
wamachinga wote ili waweze kufanya biashara katika mazingira tulivu.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati ya bunge uchumi na
biashara Mh Dunstan Kitandula amesema licha ya jitihada zinazofanywa na
wizara lakini bado kuna tatizo kubwa katika uwepo wa viwanda nchini
jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Via>>ITV
Social Plugin