Mtandao huu uliwahi kuandika habari ya nesi mmoja kuamua kuwaua wagonjwa kwa kisingizo wamekuwa wengi hivyo kufanya hivyo kutampunguzia idadi ya wagonjwa anaotakiwa kuwatibu.
Pamoja na kazi ya uuguzi kuwa ni wito lakini kuna taarifa nyingi ambazo si nzuri kwa wauguzi ambao hupewa jukumu la kuwahudumia wagonjwa lakini wengine hutumia nafasi hiyo kutesa wagonjwa kwa kuwafanyia unyanyasaji.
Hii imetokea huko Uingereza ambapo muuguzi mmoja Victorino Chua wa hospitali ya Stepping Hills amehukumiwa kwa kosa la kuwaua wagonjwa wake wawili na wengine 20 kuwawekea dripu yenye sumu kwa makusudi baada ya uchunguzi kukamilika.
Muuguzi huyo alisababisha vifo vya Tracy Arden, mwenye umri wa miaka 44, na Derek Weaver mwenye umri wa miaka 83 katika hospitali hiyo baada ya kuwazidishia dawa na mahakama kumfungulia kesi ya mauaji.
Imeelezwa wagojwa hao waliwekewa sumu hiyo mwanzoni mwa mwaka 2011 na kufariki July mwaka huo huo na hakuwa na mtu aliyehisi na sababu ya daktari huyo kufanya hivyo haikufahamika na uchunguzi unaendelea.
Social Plugin