----
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara,Mwigulu
Nchemba amejiuzulu wadhifa huo.
Mwigulu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha,ametangaza
kujiuzulu nafasi hiyo leo Jioni katika kikao cha Halmashauri Kuu ya ya Taifa ya
CCM,Mjini Dodoma
Akithibitha tukio hilo,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi
,Nape Nnauye amesema,Mwigulu ameamua kujiuzulu nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu wa
CCM-Bara kutokana na nia yake ya kutaka kuomba kuwania Urais kwa tiketi ya
CCM katika Uchaguzi utakaofanyika Octoba Mwaka huu
Mwigulu alishakuwa amemwambia nia hiyo Mwenyekiti wa
Chama Rais Jakaya Kikwete,nae Rais akamkubalia, na sasa leo katika kikao
ameomba rasmi kujiuzulu na Mwenyekiti Rais Jakaya Kikwete amemkubalia Mbele ya
wajumbe wa NEC hii leo'..amesema Nape
Social Plugin