NHIF YATOA ELIMU YA KIKOA NA KUPIMA AFYA ZA WANANCHI MAONESHO YA SIDO KANDA YA ZIWA MJINI SHINYANGA


Maonesho ya SIDO kanda ya Ziwa 2015-Kushoto ni afisa matekelezo kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Shinyanga  Katoto Mohamed akitoa maelezo kuhusu NHIF kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga aliyetembelea banda la NHIF katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga wakati wa maonesho ya 13 ya SIDO kanda ya ziwa leo Mei 30,2015 wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo kwa niaba ya waziri wa Viwanda na Biashara nchini.
 Afisa matekelezo kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Shinyanga  Katoto Mohamed akimpatia mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga kipeperushi cha huduma zinazotolewa na  NHIF.Mohamed pia alitoa ufafanuzi kuhusu mpango wa KIKOA wanaowasilisha katika maonesho hayo ya SIDO.Alisema KIKOA ni utaratibu wa utoaji wa huduma za afya kwa kadi kwa vikundi/ushirika vilivyo katika sekta isiyo rasmi.
Afisa matekelezo kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Shinyanga  Katoto Mohamed akiendelea kutoa maelezo kwa  mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga alipotembelea banda lao
Katika Banda la NHIF huduma za upimaji wa afya pia unafanyika,ambapo wananchi wanapima uzito,urefu,kisukari,presha n.k sambamba na kupatiwa ushauri.Pichani wananchi wakiwa katika foleni kupima uzito
Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika foleni kupata vipimo kutoka kwa daktari Bethy Shayo kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga

Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika foleni kupata vipimo kutoka kwa daktari Bethy Shayo kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga
Manesi kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Mektrida Ruta(kulia) na  Grace Mtunguja wakiendelea kutoa vipimo na ushauri kwa wakazi wa Shinyanga waliofika katika banda la NHIF katika viwanja vya Shycom
Vipimo na ushauri unaendelea
Afisa matekelezo kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Shinyanga  Katoto Mohamed akitoa vipimo kwa mkazi wa Shinyanga katika banda la NHIF
Zoezi la Vipimo linaendelea
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post