Afisa mkuu Udhibiti Viatarishi Vya Malengo kutoka makao makuu NHIF Thadeus Machume akitoa mada.Aliwahamasisha wadau wa afya kufika katika ofisi za NHIF kuomba mkopo kwani ni watu wachache sana wanajitokeza kuchukua mikopo hali inayofanya pesa iendelee kubaki NHIF kutokana na kukosa watumiaji huku vituo vya afya vikiendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa dawa.
Wadau wa afya wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini |
Dkt Daniel Maguja kaimu mganga mkuu mkoa wa Shinyanga akichangia mawili matatu katika semina hiyo |
Afisa mkuu Udhibiti Viatarishi Vya Malengo kutoka makao makuu NHIF Thadeus Machume akisisitiza jambo katika semina hiyo |
Maafisa kutoka NHIF wakifurahia jambo wakati Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza |
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini |
******************
Imeelezwa kuwa bado
kuna mwitikio mdogo wa vituo vya afya nchini kuchukua mikopo ya vifaa
tiba,ukarabati wa vituo,dawa na vitendanishi kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF).
Hayo yamesemwa leo na
Afisa
mkuu Udhibiti Viatarishi Vya Malengo kutoka makao makuu NHIF Thadeus Machume wakati wa kikao juu ya Uhamasishaji
juu ya Utaratibu wa Utoaji Mikopo ya Vifaa Tiba,Ukarabati wa Majengo na Dawa
kwa Vituo vya Kutolea Huduma za Matibabu kilichofanyika katika ukumbi wa mkuu
wa mkoa wa Shinyanga.
Alisema bado mwitikio ni
mdogo wa kuchukua mkopo wadau wanaotoa huduma kupitia mfuko huo jambo
ambalo ni changamoto ambayo wanaendelea kuifanyia kazi.
Alisema tangu kuanzishwa
kwa mikopo ya vifaa tiba mwaka 2008 mpaka Desemba 2014 kiasi cha shilingi
10.24 bilioni kiliidhinishwa kwa ajili ya vituo 194 vilivyoomba ni 146
vilikidhi masharti na kuchukua mkopo wa jumla ya shilingi 5.344 bilioni.
Aidha alisema kwa
upande wa mikopo ya ukarabati wa vituo vya kutolea huduma mikopo kiasi cha
shilingi 6.8 bilioni kiliidhinishwa na iliyokidhi masharti na kuchukuliwa ni
shilingi 2.14 bilioni hivyo kuwataka wadau wa afya kujitokeza kuchukua mikopo
kwani pesa ipo ya kutosha kwa ajili ya kunusuru vituo vya afya nchini.
“Vituo vingi vya afya
vina changamoto ya uhaba wa dawa,vifaa tiba na uchakavu wa majengo,lakini watu
wachache sana wanajitokeza kuchukua mikopo,tunaomba sasa mfike kwenye ofisi za
bima kwani hakuna mashari magumu wala hauhitaji kutoa rushwa ili kupata
mkopo”,alisema Machume.
Naye afisa
mdhibiti Ubora wa Afya kutoka ofisi ya Bima ya Taifa ya Afya mkoa wa Shinyanga Dkt. Gustav Kisamo ,
aliwashauri wadau hao kutumia mikopo ya vifaa tiba,madawa na vitendanishi
sanjari na ukarabati wa majengo ili kuondoa changamoto zilizopo na kuboresha
huduma kwa wagonjwa .
“Pesa huwa tunaweka
kwenye akaunti za wa kurugenzi wa halamshauri za wilaya lakini tunashauri kila
kituo cha afya kiwe na akaunti yake,vituo vya afya vinapaswa kubadilika sasa
ili kuwa msaada mkubwa zaidi kwa wananchi”,aliongeza Dkt. Kisamo.
Kwa upande wake afisa utumishi mkoa wa
Shinyanga Raymond Kiwesa alisema kutokana na kuwepo kwa changamoto ya
upatikanaji wa madawa hivyo mikopo inayotolewa na NHIF itakuwa ni fursa nzuri
kwa maslahi ya wananchi.
Katika hatua nyingine
alivitaka vituo vya huduma za afya
kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na watumishi wake kutoa kauli nzuri
kwa wateja wao ,hatua ambayo itasaidia kuongeza idadi ya wanachama wa mfuko wa
bima ya afya ya Taifa NHIF sanjari na kuboresha upatikanaji wa madawa na
vifaa tiba.
Kwa upande wake kaimu
mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Maguja alionyesha wasiwasi
juu ya mikopo inayotolewa kwa kile alichodai kutokuwa na uwazi, huku akiutaka
mfuko wa taifa wa bima ya afya kurekebisha mapungufu yaliyopo ili kuongeza
idadi ya vituo vitakavyochukua mikopo.