Inaweza hii
ikakushangaza kidogo lakini huu ndio ukweli baada ya hotel moja mjini
Tokyo Japan kuamua kuwatengenezea vyumba maalum wanawake kwa ajili ya
kulia.
Hotel hiyo inayojulikana kwa jina la Mitsui Garden Yotsuya
inasemekana imeamua kufanya hivyo ili kuwaruhusu wanawake wageni
wanaokuja hapo kulia wakiwa huru tena kwenye mazingira mazuri ambayo
hayawezi kuwasumbua.
Unaambiwa
ndani ya hotel hizo kuwa vitambaa kabisa vitakavyotumika kufuta machozi
pamoja na ‘makeup’ vipodozi ambavyo watatumia baada ya kukata kiu yao.
Pia kuna mikanda ya video yenye kusikitisha ambayo wamewekewa kwa ajili ya kuitazama ili kuwasaidia kuongeza kulia kama A moment to Remember na Forest Gump.
Gharama kwa usiku mmoja ni Yen 10,000 ambayo ni sawa na 150,000 ya Kitanzania.
Social Plugin