Shirika la AGPAHI (Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare
Initiative) linalojihusisha na mapambano dhidi ya ya Virusi vya UKIMWI na
UKIMWI linalofadhiliwa na watu wa Marekani kupitia Shirika la Kimarekani la
Center for Disease Control and Prevention(CDC) nchini Tanzania leo limezindua
majengo mawili kwa ajili ya Huduma za
Tiba na Matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI katika
zahanati ya Kagongwa wilayani Kahama na kituo cha afya cha Nindo kilichopo katika wilaya ya
Shinyanga Vijijini Mkoani Shinyanga.
Majengo hayo yamezinduliwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally
Nassoro Rufunga ambapo alisema serikali ya mkoa wa Shinyanga inatambua sana
mchango wa shirika la kitanzania la AGPAHI linalofanya kazi zake katika mkoa
huo na mikoa ya Geita na Simiyu katika jitihada zake za kupambana na VVU.
Mbali na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na AGPAHI,Rufunga
alisema majengo hayo ya kisasa yatakuwa msaada mkubwa katika kutoa huduma ya
tiba na matunzo kwa watu wote walio na maambukizi ya VVU na UKIMWI,pia huduma ya
kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Naye mkurugenzi mtendaji wa AGPAHI Lauren Rugambwa Bwanakunu
alisema katika mkoa wa Shinyanga kuna vituo 43 vinavyotoa huduma za tiba na
matunzo kwa watu wanaoishi na VVU na UKIMWI na vituo 310 vinavyotoa huduma za
kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto katika mikoa ya
Shinyanga,Simiyu na Geita.
Bwanakunu alisema lengo la kujenga majengo hayo ni kuondoa
msongamano wa wateja na kuongeza ubora wa huduma na usiri.
Shirika la AGPAHI lilianza kazi zake mwaka 2011 kwa msaada
wa watu wa Marekani kwa kusaidiana na serikali ya Tanzania.
Shirika la AGPAHI
limetokana na shirika la kimataifa la EGPAF,lililokuwa likisaidia upatikanaji
wa huduma na matunzo kwa watu wenye VVU.
Mwandishi mkuu wa Malunde1
blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa Uzinduzi wa Majengo hayo mawili katika
zahanati ya Kagongwa wilayani Kahama na kituo cha afya cha Nindo katika wilaya
ya Shinyanga vijijini,Ametuletea picha 50 Tazama hapa
chini
|
KAZI ILIANZIA KWENYE ZAHANATI
YA KAGONGWA
Hili ni jengo la huduma za tiba
na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU na UKIMWI katika zahanati ya Kagongwa
lililopo katika halmashauri ya mji Kahama,limejengwa na Shirika la AGPAHI linalofadhiliwa
na watu wa Marekani kupitia Shirika la Kimarekani la Center for Disease Control
and Prevention(CDC).
|
|
Mganga
mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe akizungumza wakati wa uzinduzi huo
ambapo alisema uwepo wa jengo hilo utasaidia wakazi wa eneo hilo na maeneo ya
jirani kuwa na ari ya kupima afya zao na kupata matibabu mbalimbali. |
|
Dkt
Kapologwe alisema mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa yenye ushamiri mkubwa
wa maambukizi ya VVU na UKIMWI ambapo sasa maambukizi ni asilimia 7.4. |
|
Mkurugenzi
mtendaji wa AGPAHI Lauren Rugambwa Bwanakunu akizungumza katika zahanati ya
Kagongwa ambapo alisema zahanati hiyo ni kati ya vituo 43 vinavyopata misaada
katika huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU.
|
Alisema misaada inayotolewa na
AGPAHI ni pamoja na vitendea kazi(pikipiki),vifaa vya ofisi(viti,meza,kabati,computer,printer
n.k
|
Tunafuatilia
kinachoendelea hapa…….. | |
Mkurugenzi
mtendaji wa AGPAHI Lauren Rugambwa Bwanakunu alisema pia AGPAHI kwa
kushirikiana na wizara ya afya inawajengea uwezo watumishi wa afya kwa njia ya mafunzo.
Misaada
mingine inayotolewa na AGPAHI ni vifaa tiba(BP Mashine,PIMA
Machine,Statoscope,mizani na madawa.
|
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambapo
aliwataka wakazi wa Kahama na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi kupata
huduma zinazotolewa katika zahanati ya Kagongwa ambayo baadaye itapandishwa
hadhi na kuwa kituo cha afya. |
|
Kikundi
cha maigizo kikitoa somo na burudani |
|
Jengo
hili lina vyumba 7 vya kutolea huduma na sehemu ya kusubiria.Vyumba vine ni vya
waganga,kimoja cha dawa,kuna cha nasaha na kingine ni masjala. |
|
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizindua/akifungua jengo hilo. | |
|
Kilichokuwa kinasomeka ukutani-Zahanati
hiyo pia imeweza kuwaanzishia dawa wateja wapatao 1,819( wanaume 716 wanawake
1,103) ,na kwenye matunzo kati yao watoto ni 129 sawa na 7%. |
|
Mkurugenzi
mtendaji wa AGPAHI Lauren Rugambwa Bwanakunu akishiriki uzinduzi wa jengo hilo. |
|
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akijiandaa kukata utepe |
|
Tabibu
wa zahanati ya Kagongwa James Bundala akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa
Shinyanga Ally Rufunga katika chumba cha masjala katika jengo hilo. |
|
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akiwa katika chumba cha Nasaha katika jengo
la Huduma za Tiba na Matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI katika
zahanati ya Kagongwa wilayani Kahama. |
|
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akisisitiza jambo katika moja ya vyumba vya
jengo hilo la kisasa. |
|
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga na viongozi mbalimbali wa mkoa,wilaya na
AGPAHI wakielekea jukwaa kuu baada ya kuzindua jengo hilo. |
|
Watumishi
wa zahanati ya Kagongwa wakicheza |
|
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akitoa hotuba yake ambapo alitoa wito kwa
wazazi ambao watoto wao wamepatwa na maradhi ya UKIMWI wawapeleke kuwaandikisha
pia wao wenye kujiandikisha kwenye huduma zinazotolewa katika kituo hicho na
kuhudhuria kliniki mara kwa mara. |
|
Wakazi
wa Kagongwa wakiwa eneo la tukio |
|
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambapo
alisema AGPAHI wamekuwa msaada mkubwa kwa katika utoaji huduma za afya mkoani
Shinyanga. |
|
Watumishi katika zahanati ya
Kagongwa wakiwa wamesimama-Hawa ni miongoni mwa watumishi walionufaika na
mafunzo mbalimbali yanayotolewa na AGPAHI katika kuwajengea uwezo kuhusu mambo
ya afya.
|
|
Hadi
mwezi Machi 2015,zahanati ya Kagongwa imeweza kuandikisha wateja 3001( wanaume
1,155 na wanawake 1,846) kati yao watoto ambao wako chini ya miaka 15 ni 186
sawa na 6.2%. |
|
Picha
za pamoja na mkuu wa mkoa wa Shinyanga zikaanza kupigwa |
|
Upigaji picha za pamoja
Unaendelea
|
|
Picha
ya kumbukumbu |
|
KAZI IKAENDELEA KATIKA WILAYA
NYINGINE_HAPA NI KATIKA WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI KATIKA KITUO CHA AFYA NINDO
UZINDUZI WA JENGO UMEFANYIKA PIA.
Hili
ni jengo la Huduma za Tiba na Matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI
na UKIMWI katika cha afya cha Nindo kilichopo katika kata ya Iselamagazi wilaya
ya Shinyanga Vijijini Mkoani Shinyanga,ambalo pia lina vyumba 7 kama jengo la zahanati Kagongwa wilayani Kahama.
|
|
Katibu
tawala wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo hilo ambapo
aliliomba shirika la AGPAHI kuendelea kutoa msaada kwa wakazi wa Shinyanga kwani wanapata manufaa mengi. |
|
Mbunge
wa jimbo la Solwa Ahmed Salum akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambapo
alipongeza kazi ya AGPAHI katika kuwafikia wananchi huku akitoa ahadi ya
kuendelea kushirikiana na shirika hilo katika kujali afya za wakazi wa jimbo
lake. |
|
Mganga
mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe akizungumza katika kituo cha afya
cha Nindo. |
|
Hadi
kufikia mwezi Machi,2015,kituo cha afya cha Nindo kimeweza kufikiwa na wateja 1379(
wanaume 532,wanawake 847) na kwenye huduma ya matunzo kati yao watoto ni 80
walio chini ya miaka 15 sawa na 6%. |
|
Hiki
ni choo kilichojengwa na AGPAHI katika kituo cha afya cha Nindo katika wilaya
ya Shinyanga. |
|
Muonekano wa jengo hilo la
kisasa
|
|
Kikundi
cha kwaya ya Mshikamano wakiimba wimbo kuhusu UKIMWI |
|
Mbunge
Ahmed Salum akicheza na kikundi
cha wahamasishaji kuhusu masuala mbalimbali
kuhusu UKIMWI. katika kituo hicho cha afya cha
Nindo. |
|
Mkurugenzi
mtendaji wa AGPAHI Lauren Rugambwa Bwanakunu akizungumza katika kituo cha afya
cha Nindo ambapo aliwataka wanaume kubadili tabia na kuwa tayari kupimwa afya
zao wakiwa pamoja na wenzi wao ili kuzuia maambukizi ya VVU kwa watoto
wanaozaliwa kwani baba na mama watakuwa wanajua afya zao kabla ya kuamua kupata
mtoto. |
|
Jukwaa
kuu, tunafuatilia kinachoendelea.... |
|
Wakazi
wa Iselamagazi wakiwa eneo la tukio |
|
Mkurugenzi
mtendaji wa AGPAHI Lauren Rugambwa Bwanakunu akifurahia jambo na mbunge Ahmed Salum |
|
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akizindua jengo
katika kituo cha afya cha Nindo lililojengwa kwa ufadhili wa Centers For Desease Control and Prevention |
|
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akikata utepe katika jengo hilo |
|
Sista Emelda Misana,ambaye ni
muuguzi mkunga katika kituo cha afya cha Nindo akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa
wa Shinyanga Ally Rufunga katika chumba cha nasaha.
|
|
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akiangalia TV iliyopo katika eneo la
kusubiria huduma katika kituo cha afya cha Nindo wilaya ya Shinyanga vijijini. |
|
Wanenguaji wa kikundi cha Ukombozi kinaimba nyimbo za asili wakifanya yao |
|
Burudani inaendelea |
|
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akitoa hotuba yake ambapo aliwataka viongozi wa wilaya kuhakikisha
kuwa majengo hayo yanatunzwa na kufanyiwa ukarabati ili yaweze kudumu kwa muda
mrefu. |
|
Baada ya uzinduzi ,picha
za kumbukumbuku |
|
Picha za kumbukumbuku |
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin