ANGALIA PICHA-KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI KITAIFA MKOANI SHINYANGA
Tuesday, May 12, 2015
Ikiwa leo ni Mei 12,2015 Kilele cha maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani kimefanyika kitaifa mkoani Shinyanga katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa makamu mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii nchini Dkt Seif Rashid.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga wakiwemo viongozi wa Chama cha Wauguzi Tanzania,waganga wakuu wa mikoa na wilaya,muuguzi mkuu wa serikali,Viongozi wa baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania,wakuu wa wilaya,wauguzi wa mikoa na wilaya,wanafunzi wa vyuo vya uuguzi,wadau wa afya n.k .
Hii ni siku maalum kwa taaluma ya Uuguzi ambayo ni maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muasisi wa taaluma ya uuguzi duniani bi Frolence Nightingale.
Wauguzi nchini Tanzania wamegawanyika katika fani mbalimbali katika kutoa huduma kwa jamii,ikiwa ni pamoja na wauguzi wakunga,wauguzi afya ya akili,wauguzi afya ya jamii,wauguzi wa magonjwa ya watoto,wauguzi wa magonjwa ya macho,wauguzi wa nusu kaputi na wauguzi walimu,watafiti,watunga sera,meneja n.k.
Wakizungumza katika maadhimisho hayo wauguzi hao walipaza sauti juu ya changamoto wanazokabiliana nazo kama vile upungufu mkubwa wa wauguzi,ukosefu wa nyumba za kuishi wauguzi,uhaba na ubora wa vitendea kazi,msongamano wa wagonjwa wodini,muundo wa utawala sekta ya afya,muundo wa utumishi wa uuguzi na ufadhili kwa wanafunzi wa uuguzi na posho mbalimbali. Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog ,Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio ametuletea picha za tukio zima la maadhimisho hayo,ANGALIA HAPA CHINI
Wauguzi kutoka halmashauri za wilaya za mkoa wa Shinyanga wakiwasili katika viwanja vya Shycom wakitokea katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga wakiwa wamebeba mabango yaliyobeba ujumbe wa kila aina
Hawa ni wauguzi kutoka Kahama
Wauguzi kutoka hospitali ya Williamson Diamonds iliyopo Kishapu wakiwa wamebeba bango wakiomba Maslahi ya wauguzi yaboreshwe
Wauguzi kutoka wilaya ya Ushetu wakiwa wamebeba bango
Wauguzi kutoka Manispaa ya Shinyanga hawakuwa nyuma
Wauguzi wakifurahia siku yao
Wauguzi kutoka manispaa ya Shinyanga wakiandamana
Maandamano yakiendelea
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe akikaribisha wageni waalikwa baada ya maandamano kupokelewa
Wanakwaya kutoka Chuo Cha Uuguzi Kahama wakitoa burudani
Wauguzi wakifuatilia kilichokuwa kinajiri
Wimbo wa wanakwaya wa Kahama ulikuwa mzuri sana ,Kulia ni mgeni rasmi makamu mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii nchini Dkt Seif Rashid akicheza baada ya mzuka kupanda
Wanafuatilia kinachoendelea uwanjani Mcheza ngoma ya Wagoyangi akicheza na nyoka karibu na meza kuu
Meza kuu wakifurahia burudani
Muuguzi mkuu wa serikali Dkt Ama Kasangala akitoa salamu za serikali kuhusu maadhimisho hayo Wauguzi wakiwa wamesimama eneo la tukio
Rais
wa Chama Cha Wauguzi nchini(TANNA) Dkt Paul Mashauri akizungumza wakati wa kilele cha
maadhimisho ya siku ya Wauguzi duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Shinyanga
Msanii kutoka kundi la Medical Culture la mjini Shinyanga akitoa burudani
Msanii akifanya yake
Wauguzi wakijiandaa kuwasha mshumaa ikiwa ni ishara ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muasisi wa taaluma ya uuguzi duniani bi Frolence Nightingale
Wauguzi wakiwa wamebeba mishumaa
Mgeni rasmi mgeni rasmi alikuwa makamu mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii nchini Dkt Seif Rashid akijiandaa kuwasha mshumaa
Mgeni rasmi makamu mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii nchini Dkt Seif Rashidakiwasha mshumaa
Wauguzi wakila kiapo kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi yao
Wauguzi wakiapa
Kwaya ya AIC Shinyanga wakitoa burudani
Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akitoa salama za manispaa ya Shinyanga
Mgeni rasmi makamu mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii nchini Dkt Seif Rashid akitoa hotuba
Kwaya ya wanafunzi wa chuo cha Uuguzi Kolandoto wakitoa burudani
Mgeni
rasmi makamu mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii nchini Dkt Seif Rashid akitoa zawadi kwa makundi mbalimbali katika sekta ya afya mkoani Shinyanga yaliyofanya vyema katika utoaji huduma za afya
Wauguzi kutoka halmashauri ya wilaya ya Ushetu wakimpongeza mfanyakazi mwenzao aliyepata zawadi ya ufanyakazi bora
Wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi Kolandoto wakifurahia zawadi aliyopewa mwalimu wao
Wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi Kahama wakimpongeza mwalimu wao kupewa zawadi ya mwalimu bora
Mgeni
rasmi makamu mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii nchini Dkt Seif Rashidakimpa zawadi ya ufanyakazi bora mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe
Wafanyakazi wa mkoa wa Shinyanga wakimpongeza mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe kwa kupata zawadi
Wakati maadhimisho yanaendelea,wanafunzi wakatumia fursa hiyo kutembelea banda la maonesho ya taaluma ya uuguzi katika viwanja vya Shycom
Wakazi wa Shinyanga wakiingia kwenye banda la Intrahealth International kupima afya zao ili kujua kama wana maambukizi ya VVU ama la!!
Social Plugin