Chozi la Binti
Kibena,ni filamu ya Kitanzania yenye lengo la kufichua vitendo vya kikatili
vinavyofanywa kwa watoto hususani wa kike, mfano wa vitendo hivyo kama vile unyanyasaji
wa kijinsia,ubakaji,ndoa za utotoni na vingine vingi.
Maudhui ya Filamu hii
kwa kiasi kikubwa yamejikita katika kukemea ndoa za utotoni ambapo vyanzo
mbalimbali vya ndoa za utotoni,athari na madhara anayoyapata mtoto anayeolewa
angali mdogo vimebainishwa.
Filamu ya Chozi la
binti Kibena imeandikwa na Amani Masuka na
kutayarishwa na Dr. Monica
Muhoja Edutaiment Centre (MOMEC),mpiga picha akiwa ni Amani Masuka,
na kuhaririwa na
Amani Masuka na Baraka Makaba
na Muongozaji ni
Dennis Sweya (Dino).
Ndani ya filamu ya
CHOZI LA BINTI KIBENA utakutana na Kisa cha kusisimua chenye
kuhuzunisha,kufundisha na kuburudisha kinachomuhusu Tunu,(Binti Kibena).
Pia Utakutana na
wasanii wakongwe kama Riyama Ally, Dennis Sweya Dino, Lutwaza Philmon (The Next
Kanumba) Nassoro Ndambwe nk.
Pia filamu hii
imeibua vipaji vipya kama Maria Sweya (Tunu) alie vaa uhusika mkuu na kufanya
mambo makubwa kiasi ambacho kilimshangaza Riyama Ally aliyecheza naye kama mama
yake wa kufikia.
Wengine ni Bity,Tid
Clever,Irene Kitaa,Gema Isack,Hans Chamoto nk.
Filamu hiyo ya
Kihistoria imeshakamilika kinachosubiriwa sasa ni tarehe rasmi ya
uzinduzi,ambapo watanzania watapata wasaa mzuri kabisa wa kuiona kwenye jumba
la sinema kisha mtaani.
MOMEC inawashukuru
wadau wote walio iwezesha filamu hiyo kukamilika katika ubora wa kimataifa na inawaomba
watanzania kuipokea kwa mikono miwili kwani watapata kitu ambacho kitakata kiu
yao ama kitawapa mtazamo mpya wa level za kimataifa.
TAZAMA BAADHI YA PICHA KATIKA FILAMU HIYO HAPA CHINI
Social Plugin