Askari polisi wa FFU wakiwadhibiti waendesha bodaboda mjini Shinyanga-Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog Waendesha bodaboda wakiwa barabarani |
Askari polisi wakiwa barabarani kuzuia waendesha bodaboda wasizuie magari
|
Askari polisi wakiwa eneo la tukio-picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog |
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida jeshi la polisi mkoani Shinyanga limelazimika kutumia
mabomu ya machozi kuwatawanya waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda baada ya
kuandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga kasha kufunga barabara kuu ya kutoka Mwanza kuelekea
Tabora wakidai wamechoka kuonewa na jeshi hilo.
Vurugu
hizo zimetokea leo saa tano asubuhi ambapo waendesha pikipiki hao waliandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga,
ili kuwasilisha kero zao za jeshi la polisi, ambapo wamekuwa wakiwaonea bila ya
kufuata sheria, na kuwafanya kuwa kama vitega uchumi vyao.
Kutokana
na hali hiyo askari wa jeshi la polisi walitanda katika ofisi za mkuu wa mkoa
wa Shinyanga kukabiliana na bodaboda hao ambao baada ya zoezi la kumuona mkuu
wa mkoa kushindikana waliamua kufunga
barabara kuu itokayo Mwanza kuelekea Tabora.
Kufuatia
kitendo cha kuzuia mabasi kwa muda hali hiyo iliyolazimu
jeshi la polisi kuingilia kati na kuwatawanya na
ndipo
walipochukua sheria mkononi na kuanza kuwarushia mawe askari hao kitendo
kilichosababisha kuanza kurusha mabomu na kuanza kuwapiga na virungu.
Waendesha
bodaboda hao amesema ,askari hao hasa wanaotembea na pikipiki barabarani
maarufu kama (Makhirikhiri),wamekuwa wakiwanyanyasa kwa kuwakamata hovyo, huku
wakiwavizia kwenye kona na kwamba licha ya kuviziwa kwenye kona wamekuwa
wakiwavamia vijiweni huku wakiwa wamepaki pikipiki na kuzifunga minyororo,
kuwatoza stika za wiki ya usalama barabara ambazo muda wake umeshapita.
Wamedai
kuwa askari haowamekuwa wakiwakimbiza na kuwachapa fimbo migongoni, pamoja na
kuwaomba rushwa mara wanapo wakamata licha ya kuwakuta hawana makosa.
Na Marco Maduhu-Malunde1 blog |
Social Plugin