Kampuni ya Uchimbaji madini ya ACACIA mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo Kahama leo imetoa msaada wa magodoro 60 yenye thamani ya shilingi milioni 7 na nusu kwa ajili ya wazee wanaolelewa katika kituo cha Kolandoto kilichopo katika manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Magodoro hayo 60 yamekabidhiwa na meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Philbet Rweyemamu kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga katika ofisi ya mkuu huyo wa mkoa mjini Shinyanga.
Akizungumza wakati wa kukabidhi magodoro hayo meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Philbet Rweyemamu amesema wameamua kutoa msaada huo kupitia sera yao ya kuhakikisha kwamba wanakuwa wachangiaji wazuri katika jamii wanayoishi nayo kupitia mfumo wao wa “Tufanikiwe Pamoja”.
Rweyemamu amesema msaada huo ni sehemu ya juhudi zao za kuhakikisha kwamba mafanikio yao kama kampuni yanatafsiriwa kivitendo katika jamii.
Ameongeza kuwa magodoro hayo yatatumika kutatua changamoto ya uhaba wa magogoro unakikabili kituo cha wazee cha Kolandoto huku akitaka magodoro hayo kuwafikia walengwa na kutumika kama inavyotakiwa.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ameushukuru mgodi wa Buzwagi kwa kutoa msaada huo huku akiwaomba wadau mbalimbali kuendelea kusaidia makundi mbalimbali ya watu yanayohitaji msaada ikiwemo watoto wenye ulemavu wanaolelewa katika kituo cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.
Rufunga amesema vituo vya wazee na watoto wenye ulemavu vya Buhangija na Kolandoto vinakabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo ni vyema wadau wakaendelea kusaidiana na serikali katika kukabiliana nazo.
Msaada huo wa magodoro unatokana na wazo la kampuni ya Easyflex Production inayojihusisha uzalishaji na usambazaji wa Video na Sauti ya mjini Shinyanga iliyoendesha harambee mwezi Mei mwaka jana kwa ajili ya kusaidia Vituo vya Kulelea Watoto wenye ulemavu na Wazee wasiojiweza mkoani Shinyanga ambapo Mgodi wa Buzwagi uliahidi kutoa msaada wa magodoro ahadi ambayo wameitekeleza.
Malunde1 blog ilikuwepo wakati wa makabidhiano hayo,angalia picha hapa chini
Awali lori lililosheheni magodoro yaliyotolewa na Kampuni ya ACACIA mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama mkoani Sinyanga likiwasili katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga mjini Shinyanga
Nje ya ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga- Zoezi la kushusha magodoro kutoka kwenye gari likachukua nafasi
Magodoro yanaendelea kushushwa
Magodoro 60 yenye thamani ya shilingi milioni 7 na nusu baada ya kushushwa tayari kabisa kwa ajili ya meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Philbet Rweyemamu kuyakabidhi kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga.
Kushoto ni meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Philbet Rweyemamu akiwa na Afisa Mahusiano mgodi wa Buzwagi Dorothy Bikurakule wakiwasili eneo la Makabidhiano
Katikati ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga kuelekea kwenye eneo la makabidhiano.Kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro
Eneo la Makabidhiano-Kushoto ni Afisa Mipango mkoa wa Shinyanga George Andrew akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi Magodoro hayo 60 kwa ajili ya wazee wa Kolandoto.Katikati ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akifuatiwa na meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Philbert Rweyemamu
Kulia ni meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Philbert Rweyemamu akizungumza wakati wa kukabidhi magodoro hayo ambapo alisema msaada huo ni sehemu ya sera yao ya kuhakikisha kuwa wanashirikiana na jamii inayowazunguka katika mfumo wa "Tufanikiwe Pamoja"
Meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Philbert Rweyemamu alisema mgodi wake utaendelea kusaidia jamii ikiwa ni sehemu ya juhudi zao za kuhakikisha kwamba mafanikio yao kama kampuni yanatafsiriwa kivitendo katika jamii.
Meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Philbert Rweyemamu akishikana mkono na mkuu wa mkoa wa Shinyanga wakati akikabidhi magodoro hayo 60 kwa ajili ya wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga
Eneo la makabidhiano,zoezi likiendelea
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akishikana mkono na meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Philbert Rweyemamu wakati wa mabidhiano
Kulia ni meneja Uendelevu mgodi wa Buzwagi George Mkanza,akifuatiwa na mkurugenzi wa kampuni ya Easyflex Production inayojihusisha uzalishaji na usambazaji wa Video na Sauti ya mjini Shinyanga Happiness Mwaja Kihama iliyoendesha harambee mwezi Mei mwaka jana kwa ajili ya kusaidia Vituo vya Kulelea Watoto wenye ulemavu na Wazee wasiojiweza mkoani Shinyanga,kushoto kwake ni Afisa Mahusiano mgodi wa Buzwagi Dorothy Bikurakule
Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizungumza baada ya kupokea magodoro hayo ambapo aliushukuru mgodi wa Buzwagi kwa kutoa msaada huo huku akiwaomba wadau mbalimbali kuendelea kusaidia makundi mbalimbali yanayohitaji msaada ikiwemo watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa katika kituo cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.
Kushoto ni Afisa Mahusiano mgodi wa Buzwagi Sophia Chikira akichukua matukio yaliyokuwa yanajiri eneo la tukio
Mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizungumza katika eneo la tukio
Baada ya kupokea magodoro hayo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga naye alikabidhi magodoro hayo kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (Kushoto) kwa ajili ya kuyafikisha kwa wazee zaidi ya 40 wanaolelewa katika kituo cha Kolandoto.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akikabidhi magodoro hayo kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro atakayepeleka magodoro hayo kwa walengwa akiwa ameambatana na mkurugenzi wa kampuni ya Easyflex Production Happiness Mwaja Kihama
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akikabidhi magodoro hayo kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Hapa ni Ndani ya Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga-Zoezi la kusainishana hati ya makabidhiano ya magodoro kati ya mgodi wa Buzwagi na ofisi ya mkoa wa Shinyanga likaendelea
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akisaini hati ya makabidhiano ya magodoro
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi Philbert Rweyemamu akishikana mkono na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga baada ya kusaini hati ya makabidhiano
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizungumza baada ya zoezi la kusaini hati ya makabidhiano
Baada ya makabidhiano picha ya pamoja ikapigwa:Wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Festo Kang'ombe,akifuatiwa na fisa Mipango mkoa wa Shinyanga George Andrew,Afisa Mahusiano mgodi wa Buzwagi Dorothy Bikurakule ,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga.Wa kwanza kushoto ni afisa mahusiano mgodi wa Buzwagi Yunia Wangoya,akifuatiwa na mkurugenzi wa kampuni ya Easyflex Production Happiness Mwaja Kihama,meneja Uendelevu mgodi wa Buzwagi George Mkanza na meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Philbet Rweyemamu
Picha za kumbukumbu zikaendelea kupigwa
Wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi wakijiandaa kurudi wilayani Kahama baada ya kumaliza zoezi la kukabidhi msaada wa magodoro 60 kwa ajili ya wazee wasiojiweza katika kituo cha Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga.Pichani ni dereva wao bwana Mayombo akitafakari jambo kabla ya kuanza safari
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Social Plugin