Serikali imeahidi kumchukulia Shilole kufuatia kusambaa kwa picha zake chafu zilizopigwa wakati
akitumbuiza nchini Ubelgiji.
Akizungumza bungeni Dodoma leo, Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma
Mkamia, wakati akijibu hoja za wabunge baada ya kusoma makadirio na matumizi wa wizara hiyo,
alisema tayari serikali imeliagiza baraza la sanaa taifa BASATA kufanya naye mahojiano.
Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia
“Tumemtaka ajieleze kupitia BASATA, akishajieleza serikali itachukua hatua na niombe
mheshimiwa spika kupitia bunge lako tufuku, kuliomba radhi kwa upande wa serikali kwa kitendo
kilichofanywa na mwanamuziki yule. Sio maadili yetu na nimesema akishajieleza serikali itachukua
hatua yake,” alisema Juma Mkamia.
Social Plugin