Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete amewataka viongozi wa CCM
kuweka tofauti zao pembeni na kuhakikisha wanapitisha majina ya wagombea
wenye sifa na wanaokubalika na wananchi kwenye uchaguzi mkuu ujao ili
kukiwezesha chama hicho kushinda kwa kishindo.
Mwenyekiti huyo ametoa angalizo hilo wakati akifungua mkutano mkuu
wa halmashauri kuu ya CCM {NEC} ambapo ameonya endapo viongozi wa chama
hicho watapitisha majina ya wagombea kwa utashi wao na kusahau kuwa
nguvu kubwa ya ushindi iko kwa wananchi ambao ndio wengi, chama hicho
kisitarajie kuibuka na ushindi mkubwa kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Awali kabla ya Rais Kikwete kufungua NEC kamati kuu CCM imefanya
tathmini ya mwenendo wa mchakato zoezi la upigaji wa kura ya maoni ya
katiba mpya na kuitaka serikali kujadiliana na tume ya taifa ya
uchaguzi NEC ili kuangalia namna ya kutatua changamoto zinazolikabili
zoezi hilo ambazo zinaweza kuwa kikwazo kwa kura hiyo kwenda sambamba na
uchaguzi mkuu ujao kama ilivyotangazwa awali.
Kamati hiyo ambayo inalazimika kukaa kwa siku mbili mfululizo
kinyume na ratiba iliyotolewa awali ya siku moja kinatoa ushauri huo
baada ya kupitia hoja mbalimbali ambapo pamoja na mambo mengine imebaini
zoezi la upigaji kura ya maoni ya katiba mpya linakbiliwa na changamoto
lukuki zikiwemo kasi ndogo ya uandikishaji wa daftari la kudumu.
Changamoto zingine zilizobainishwa kuikabili kura hiyo ni pamoja na
matakwa ya kisheria ambayo yanaelekeza zoezi hilo liende pamoja na
utoaji wa elimu kwa wananchi kwa siku 60 siku 30 za kampeni na baada ya
hapo ndipo ipigwe kura ya maoni ambapo tathmini inaonyesha hakutakuwepo
na muda wa kutosha kabla ya tarehe 25 October inayotajwa kuwa ndio
tarehe rasmi ya uchaguzi mkuu.
Katika hatua nyingine wakati macho na masikio ya watanzania
yakielekezwa hapa dodoma katika vikao vya juu vya CCM vinavyotajwa kuwa
dira ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu itv inazungumza na baadhi ya
wajumbe ambao wanakiri hamasa na matumaini ni makubwa kwa mustakabali wa
chama hicho katika kukamata dola .
Via>>ITV
Social Plugin