|
Hizi ni miongoni mwa nyumba 50 za gharama nafuu zilizojengwa
na shirika la nyumba la taifa (NHC) katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula
katika halmashauri ya Mji Kahama mkoani Shinyanga.Leo Mei 29,2015 Waziri wa
Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi ameweka jiwe la
msingi katika nyumba hizo.
Mwandishi mkuu wa Malunde1
blog,ndugu Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio,ametuletea Picha 25 za
tukio zima,ANGALIA HAPA CHINI
|
|
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi(aliyevaa miwani) akiweka jiwe la msingi katika nyumba hizo zilizojengwa na NHC wilayani Kahama mkoani Shinyanga |
|
Kaimu mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki kutoka Shirika la nyumba la taifa Haikamen Mlekio akitoa maelezo kwa waziri Lukuvi kuhusu mradi
huo wa nyumba 50 wilayani Kahama ulioanza kujengwa mwezi Januari mwaka 2015 na
kutarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2015. |
|
Mradi huo wa nyumba 50 utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 2.1 na kila nyumba ina vyumba vitatu. |
|
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi akikata utepe,kulia kwake ni kaimu
mkurugenzi mkuu wa Shirika la nyumba la taifa Felix Maagi |
|
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi akiwa ndani ya moja ya majengo hayo,wa kwanza kushoto ni kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la nyumba la taifa Felix Maagi |
|
Wa pili kulia ni kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la nyumba la taifa Felix Maagi akitoa maelekezo kwa waziri Lukuvi baada ya kukagua moja ya majengo hayo 50 yaliyojengwa na NHC |
|
Meza kuu-Lengo
la NHC kujenga nyumba ni kuleta mvuto
kwa miji yetu,kupandisha hadhi ya maeneo lakini pia kuwapatia wananchi wa
kipato cha chini nyumba bora na gharama nafuu
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi akiteta jambo na mbunge wa jimbo la Kahama mjini James Lembeli |
|
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson akizungumza eneo la tukio.Alilipongeza shirika la nyumba la taifa kwa kujenga nyumba za kisasa na imara,huku akipongeza pia kitendo cha NHC kutoa msaada wa mashine za kufyatulia matofali katika halmashauri za wilaya
Eneo la tukio |
|
Kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la nyumba la taifa Felix
Maagi akizungumza eneo la tukio,alisema mradi huo wa nyumba za Kahama ni muendelezo wa utekelezaji wa
mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu nchini ikiwa ni miongoni mwa maeneo 29 ya
halmashauri mbalimbali za miji.
|
|
Kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la nyumba la taifa Felix Maagi, alisema
mradi huo wa umetengeza ajira za moja kwa moja 290,ajira shirikishi 145,makazi
ya watu 300 na utanufaisha wananchi wa Kahama wakiwemo wafanyabiashara. |
|
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi akiwahutubia wakazi wa Kahama katika eneo la mradi wa nyumba 50 zilizojengwa na shirika
la nyumba la taifa (NHC) katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula wilayani
Kahama.
Tunamsikiliza waziri Lukuvi....
|
|
Waziri Lukuvi pamoja na mambo mengine alizitaka halmashauri za wilaya kupima maeneo ya miji na kuyagawa kwa wananchi kwa utaratibu unaotakiwa ili kuondoa migogoro ya ardhi na kuweka mipango ya miji vizuri. |
|
Wananchi wakimsikiliza waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi,ambaye alisema wananchi watakaonunua nyumba za shirika la nyumba la
taifa hivi sasa kuna utaratibu wa kupatiwa hati miliki hata kama nyumba iko juu
ya ghorofa ili kuwarahisishiwa kupata mahitaji mengine muhimu ikiwemo mikopo.
Tunafuatilia kinachoendelea.....
|
|
Kundi la sanaa la Makhirikhiri wa Kahama wakitoa burudani
Nyumba moja inauzwa shilingi milioni 49 na tayari watu mbalimbali wamejitokeza kununua nyumba hizo za kisasa |
|
Kundi la Makhirikhiri likitoa burudani |
|
Kiongozi wa kundi la sanaa la Makhirikhiri Kahama akishikana mkono na viongozi akiwemo Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi |
Wananchi wakiwa eneo la tukio
Mbunge wa jimbo la Kahama Mjini James Lembeli akizungumza katika eneo la mradi ambapo aliwataka
wakazi wa Kahama kuchangamkia fursa ya nyumba hizo kwa kuanzisha miradi
mbalimbali ikiwemo ya kibiashara katika eneo hilo ili fedha za watu watakaoishi
hapo zisitoke nje ya eneo hilo.
|
Wananchi wakiwa eneo la tukio |
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com