SILAA_" AKINA MAMA MSIWAKIMBIE KINA BABA KUNA BARIDI

Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, ametoa mpya baada ya kuwataka  akina mama wasiwakimbie wenzi wao wakati huu wa baridi kwa sababu wanajenga hospitali maalumu ya mama na mtoto.
 
Hospitali hiyo itakayokuwa na vitanda 200, itajengwa eneo la Chanika kwa msaada wa watu wa Korea.

Akizungumza mwishoni mwa wiki na wakazi wa Mtaa wa Mbondole, Kata ya Msongola, Meya huyo alisema msaada huo aliuomba mwenyewe na kwamba wakati wowote kuanzia sasa ujenzi huo utaanza.
 
Alisema tayari mkandarasi, kampuni ya CM Multiworks, amepewa kazi ya kujenga zahanati ya Mbondole ambayo itagharimu Sh milioni 35.
 
“Naona wakazi wa huku ni hodari sana, maana kila ninayemuona ana mtoto, hivyo kipupwe cha mwaka huu mambo yote mwisho Chanika…akinamama msiwakimbie kina baba,” alisema Silaa.
 
Awali Diwani wa Kata ya Msongola, Angelina Malembeka, alisema eneo la ujenzi wa zahanati ya Mbondole, lenye ukubwa wa ekari mbili, limetolewa na mmoja wa wakazi wa mtaa huo, Hussein Katundu.
 
“Tunamshukuru aliyekubali kutoa eneo lake kwa ajili ya ujenzi huu, naomba watu wengine muige mfano huu kwa kutoa maeneo yenu kwa ajili ya huduma za jamii,” alisema.
 
Alisema wakati mwingine gharama za kununua eneo huwa kubwa kuliko gharama za ujenzi wa zahanati husika, hivyo akashauri watu wengine wajitolee ili kusaidia jamii.
 

Alisema zahanati hiyo itakapokamilika itaifanya kata hiyo kuwa na zahanati tatu.  Zanahati nyingine ni Mvuleni na Kiboga.

Via>>Kigoma24

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post