Meya
wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, ametoa mpya baada ya kuwataka akina
mama wasiwakimbie wenzi wao wakati huu wa baridi kwa sababu wanajenga
hospitali maalumu ya mama na mtoto.
Hospitali hiyo itakayokuwa na vitanda 200, itajengwa eneo la Chanika kwa msaada wa watu wa Korea.
Akizungumza
mwishoni mwa wiki na wakazi wa Mtaa wa Mbondole, Kata ya Msongola, Meya
huyo alisema msaada huo aliuomba mwenyewe na kwamba wakati wowote
kuanzia sasa ujenzi huo utaanza.
Alisema
tayari mkandarasi, kampuni ya CM Multiworks, amepewa kazi ya kujenga
zahanati ya Mbondole ambayo itagharimu Sh milioni 35.
“Naona
wakazi wa huku ni hodari sana, maana kila ninayemuona ana mtoto, hivyo
kipupwe cha mwaka huu mambo yote mwisho Chanika…akinamama msiwakimbie
kina baba,” alisema Silaa.
Awali
Diwani wa Kata ya Msongola, Angelina Malembeka, alisema eneo la ujenzi
wa zahanati ya Mbondole, lenye ukubwa wa ekari mbili, limetolewa na
mmoja wa wakazi wa mtaa huo, Hussein Katundu.
“Tunamshukuru
aliyekubali kutoa eneo lake kwa ajili ya ujenzi huu, naomba watu
wengine muige mfano huu kwa kutoa maeneo yenu kwa ajili ya huduma za
jamii,” alisema.
Alisema
wakati mwingine gharama za kununua eneo huwa kubwa kuliko gharama za
ujenzi wa zahanati husika, hivyo akashauri watu wengine wajitolee ili
kusaidia jamii.
Alisema zahanati hiyo itakapokamilika itaifanya kata hiyo kuwa na zahanati tatu. Zanahati nyingine ni Mvuleni na Kiboga.
Via>>Kigoma24
Social Plugin