Wananchi
katika kijiji cha Matemanga wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wanaishi kwa
hofu na kulazimika kutotembea usiku wakihofia kuliwa na simba
wanaosumbua katika kijiji hicho wakidaiwa kutoroka katika hifadhi ya
taifa ya Selou ambapo mpaka sasa wameshakula mbuzi zaidi ya
ishirini.
Wamesema simba hao wanaodaiwa kuwa watatu na wazee ambao inadaiwa
wametoroka porini baada ya kushindwa kuwinda kutokana na uzee tayari wameshakula mbuzi zaidi ya ishirini kijijini hapo.
Wamesema simba hao wamekuwa wakisumbua
katika kijiji hicho nyakati za usiku na kuwafanya waishi kwa hofu
wakihofia kuliwa na simba hao.
Mhifadhi wa wanyamapori katika wilaya ya Tunduru Charles Shawa
anasema msako mkali wa kusaka simba unaendelea huku akisema ni
simba mmoja tu ndiye anayesumbua kijijini hapo.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Chande Bakary Nalicho anasema nguvu
zimeongezwa katika msako wa simba ambapo kuna askari wanyamapori sita
katika msako wa simba.
Via>>ITV
Social Plugin