Wiki iliyopita kulikuwa na vichwa vya habari kuhusu Baraza la Sanaa Taifa kutoa barua ya Onyo kwa msanii Shilole baada ya kuonekana akiwa wazi sehemu za juu ya mwili wake jukwaani kwa bahati mbaya kwenye show yake aliyoenda kuifanya Ubelgiji.
Shilole na Snura ni watu ambao wanafananishwa na kupambanishwa na wakati mwingine kulinganishwa kwenye muziki wanaoufanya.. Snura amezungumza kuhusu ishu iliyomtokea Shilole.
Snura ameanza hivi>>’Kiukweli
kabla sijataka kusema itakuaje, mimi binafsi kutoka kwenye moyo wangu
namuombea sana msamaha na Watanzania wasimuangalie hivyo ambavyo
wanamuangalia‘
Sentensi nyingine Snura amesema>>’Ile
ni kama ajali hivyo wamuelewe kama ambavyo mwenyewe amesema yule ni mtu
mzima na ana maumivu yake ndani ya moyo kwa hiyo unapozidi kumkandamiza
ni kama unazidi kumuumiza kikubwa ni kumsamehe na kuona je itatokea
tena?‘
Social Plugin