Guo Meimei ni
mmoja ya mastaa wakubwa kwenye social network China, jina lake
limetajwa pia kuhusishwa na ishu iliyoibuka mwaka 2014 kwamba alikuwa
anaendesha genge la wahuni waliokuwa wanachezesha kamali bila kuwa na
kibali.
Tumezoea kuona kwenye kurasa za mastaa
wa kibongo kwenye mitandao ya kijamii wanaonesha nyumba zao, magari na
utajiri wao.. hata Guo Meimei nae ni staa aliyekuwa anaishi maisha ya hivyohivyo China.
Alikamatwa kwa kosa la kufungua banda la
kuchezesha kamali bila kusajiliwa, kesi iko Mahakamani na kama akikutwa
na hatia basi hukumu yake huenda ikawa miaka 10 jela.
Guo ni maarufu sana China ambako wao wanatumia zaidi mtandao wa Sina Weibo ambao uko kama Facebook na Twitter… Kama ulidhani ishu ya kamali ni kitu kidogo Sheria ya China iko hivyo na hukumu yake !!
Social Plugin