|
Katika kukabiliana na vitendo vya mauaji ya vikongwe na watu
wenye ulemavu wa ngozi(albino),leo jeshi la jadi sungusungu katika halmashauri
ya manispaa ya Shinyanga limekabidhiwa pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni moja,laki 6 na elfu 50 kwa ajili ya kuimarisha ulinzi
na usalama kwenye maeneo yao.Zoezi la makabidhiano limefanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga mgeni rasmi akiwa ni mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi
na usalama katika wilaya hiyo-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
|
|
Pikipiki hiyo imetolewa na mstahiki meya wa manispaa ya
Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam kupitia kwa mfanyabiashara Ndegesela na
kukabidhiwa kwa katibu wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga James Deshi.Pichani katikati ni meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akikabidhi ufunguo wa pikipiki kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga bi Josephine Matiro ambaye naye alikabidhi ufunguo huo kwa katibu
wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga James Deshi. |
|
Akikabidhi pikipiki hiyo meya wa manispaa hiyo Gulam Hafeez Mukadam alisema pikipiki
hiyo itatumika katika kuimarisha ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na
kukabiliana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe.
|
|
Zoezi la makabidhiano linaendelea |
|
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa zoezi la makabidhiano ambapo alisema ingawa katika manispaa hiyo
hapajaripotiwa tukio la mauaji ya albino,pikipiki hiyo itatumika katika
kuimarisha zaidi ulinzi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe. |
|
Matiro alisema wataendelea kutoa msaada wa pikipiki kwa jeshi la sungusungu katika kata 17 za manispaa hiyo na mwezi Juni mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele atatoa pikipiki 2 kwa jeshi hilo |
|
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishikana mkono na mwenyekiti wa sungu sungu manispaa ya Shinyanga Shiganza Shidula |
|
Nyuma ya pikipiki iliyokabidhiwa kwa jeshi la sungusungu
Katibu wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga James Deshi akikagua pikipiki hiyo baada ya kukabidhiwa |
|
Viongozi wa Jeshi la Sungusungu halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakiondoka na pikipiki waliyokabidhiwa,anayeendesha ni katibu wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga James Deshi-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com